TIMU
ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imepata pigo jingine baada ya
mshambuliaji wake Thomas Ulimwengu naye kuumia kifundo cha mguu.
Kuumia
kwa Ulimwengu anayekipga katika klabu ya TP Mazembe ya Jmahuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) kunafa timu hiyo kufikisha majeruhi wawili
ambapo jana, kiungo wake Nurdin Bakari alichanika nyama za paja hali
itakayomlazimu kukaa nje ya dimba kwa siku saba.
Daktari
wa Stars, Mwanandi Mwankemwa amesema Ulimwengu alipata maumivu hayo
wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wa Karume, jijini Dar es
Salaam.
Alisema
kutokana na maumivu hayo, Ulimwengu naye ataukjosa mchezo wa kimataifa
wa kirafiki dhidi ya Malawi utakaopigwa jumamosi kwenye dimba la Taifa
jijini Dar es Salaam.
Stars
inayonolewa na Mdenmark Kim Poulsen akisaidiwa na Mzalendo Sylvestre
Marsh imepiga kambi kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam
ikijiandaa mechi yake ya mchujo
kufuzu Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory
Coast itakayopigwa Abidjan Juni 2 mwaka huu. source mamapipiro blog
No comments:
Post a Comment