WADAU wa usafiri jijini Dar es Salaam, wamepinga mapendekezo ya ongezeko la nauli za daladala kutoka Sh350 hadi kufikia Sh 870. Mapendekeza hayo yaliwasilishwa na Umoja wa Wamiliki wa Daladala (Dacoboa) ambao sasa wametakiwa kujipanga upya na kuboresha huduma zao . Dacoboa, iliwasilisha mapendekezo hayo kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), ikidai kuwa gharama za uendeshaji wa biashara hiyo, zimepanda. Wakichangia maoni yao kuhusu mapendekezo hayo katika mkutano uliofanyika jana jijini Dar es Salaam, wadau walisema hakuna haja ya kupandisha nauli hizo hasa ikizingatiwa kuwa wamiliki wa daladala, wameshindwa kuboresha huduma kwa wananchi. Akizungumza katika mkutano huo, Katibu wa Baraza la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchi kavu na majini (Sumtara CCC), Raurence Simo alisema sasa si wakati mwafaka kwa wamiliki wa daladala kuongeza nauli. Alisema hiyo inatokana na ukweli kwamba mazingira ya utoaji huduma hiyo, hayajaboreshwa. Simon alisema huduma ya usafirishaji wa abiria katika Jiji la Dar es Salaam, zinatolewa chini ya viwango yakiwa ni matokeo ya wamiliki wa mabasi hayo, madereva na makondakta, kutokuwa na ujuzi wa kazi. “Madereva na makondakta hawana ujuzi wala uataalamu wa kazi hiyo, hali hiyo inasababisha msongamano, ajali na kero nyingine,”alisema Simo. “Malalamiko ya nauli yanafikia asilimia 50, lugha chafu zinazotolewa na makondakta na madereva asilimia 29 na daladala zinazokatisha njia ni asilimia 21, haya ni mambo yanayowanyima sifa za kutaka kuongezawa nauli,”alisisitiza Simo alifafanua kanuni za marejeo ya gharama za huduma za Sumatra za mwaka 2009, zinataka kampuni inayopeleka maombi ya kutaka kuongezeawa nauli, kuwasilisha mahesabu yaliyokaguliwa, taarifa ya utendaji kwa miaka iliyopita ili kuiwezesha Sumatra kujiridhisha. Katibu wa Umoja wa Madereva wa Tanzania, Salmu Abdallah, alisema wamiliki wa daladala hawapaswi kuomba kuongezewa nauli, kwa sababu watendaji wao hawana mikataba ya kazi. Alisema kuongeza nauli, kutazidi kuwanyima watendaji hao haki zao na kuwafaidisha wamiliki. “Mikataba ya kazi ambayo inawasilishwa Sumatra na wamiliki hao ni feki, wanatumia njia ya mikataba ili kupata vibali vya kuendesha bishara zao za usafilishaji na si vinginevyo” alisema. Mapema akiawasilisha sababu za kutaka kupendekeza nauli za daladala ziongezwa Mwenyekiti wa Dacoboa, Sabri Mabruki, alisema mapendekezo hayo yanatokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji wa bishara hiyo. Alisema maisha yamepanda na gharama za undeshaji wa biashara ya usafirishaji kwa sasa zimepanda, yakiwa ni matokeo ya ongezeko la bei ya mafuta. . Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra Ahmad Kilima, ufafanuzi kuhusu mapendekezo hayo yatatolewa baadaye.source gazeti la mwanaichi |
KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA CMA KWA UANZISHWAJI WA MFUMO WA KIDIJITALI.
-
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeipongeza Tume
ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa uanzishwaji wa Mfumo wa Uendeshaji na
Us...
10 hours ago
No comments:
Post a Comment