MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa
Tabora, leo inatarajia kutoa huku ya kesi ya jinai inayowakabili wabunge
wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na
wanachama wengine wawili.
Washitakiwa hao, Sylvester Kasulumbai
(Maswa Mashariki), Suzana Kiwanga (Viti Maalumu), Anuary Kashaga na
Robert William, wanabiliwa na makosa matatu ya ya kumshambulia Mkuu wa
Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, Septemba 15 mwaka jana katika kijiji
cha Isakamaliwa.
Upande wa mashitaka ulileta mashahidi
wanane akiwemo mkuu wa wilaya mwenyewe ambaye ndiye mlalamikaji, huku
upande wa utetezi ukiwa na shahidi mmoja pamoja na utetezi wao wenyewe.
Katika kesi hiyo iliyoko chini ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Thomas Simba, washitakiwa hao
kwa pamoja wanadaiwa kumweka chini ya ulinzi usio halali mkuu wa wilaya
hiyo, kisha kumtolea lugha ya matusi na kumshambulia.
Wakiongozwa na mawakili wao, Mussa
Kwikima na Mpogolo, washitakiwa hao katika utetezi wao, walikana kutenda
makosa hayo na kusema kuwa badala yake waliambiwa kwamba mkuu huyo kwa
kutumia sungu sungu, aliwazuia wananchi wasiende kwenye mkutano wa
kampeni za kugombea ubunge wa CHADEMA katika Jimbo la Igunga, zilizokuwa
zikiendelea.
No comments:
Post a Comment