Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, June 22, 2012

Hukumu kwa wabunge CHADEMA leo



MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora, leo inatarajia kutoa huku ya kesi ya jinai inayowakabili wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na wanachama wengine wawili.
Washitakiwa hao, Sylvester Kasulumbai (Maswa Mashariki), Suzana Kiwanga (Viti Maalumu), Anuary Kashaga na Robert William, wanabiliwa na makosa matatu ya ya kumshambulia Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, Septemba 15 mwaka jana katika kijiji cha Isakamaliwa.
Upande wa mashitaka ulileta mashahidi wanane akiwemo mkuu wa wilaya mwenyewe ambaye ndiye mlalamikaji, huku upande wa utetezi ukiwa na shahidi mmoja pamoja na utetezi wao wenyewe.
Katika kesi hiyo iliyoko chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Thomas Simba, washitakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kumweka chini ya ulinzi usio halali mkuu wa wilaya hiyo, kisha kumtolea lugha ya matusi na kumshambulia.
Wakiongozwa na mawakili wao, Mussa Kwikima na Mpogolo, washitakiwa hao katika utetezi wao, walikana kutenda makosa hayo na kusema kuwa badala yake waliambiwa kwamba mkuu huyo kwa kutumia sungu sungu, aliwazuia wananchi wasiende kwenye mkutano wa kampeni za kugombea ubunge wa CHADEMA katika Jimbo la Igunga, zilizokuwa zikiendelea.

No comments:

Post a Comment