Habari na Ezekiel Kamanga,Iyula Mbozi.
Hakimu
wa Mahakama ya Mwanzo,Kata ya Iyula,Tarafa ya Iyula,Wilaya ya Mbozi
Mkoani Mbeya Mheshimiwa Grace Kivelege aliuacha Ukumbi wa mahakama hyo
na kutoka nje kisha kuanza kuzozana na mwananchi mmoja Bwana Sebastian
Kilindu aliyekuwa amefika mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi.
Sababu ya ugomvi huoni pale Hakimu huyo alipomtaka mshitakiwa Bwana
Laurence Julias,kuingia mahabusu ndipo Bwana Kilindu alipinga hali
iliyompelekea hakimu kumkunja shingoni na kuamuliwa na mwandishi wa
habari hizi,huku wananchi wakishangilia zogo hilo wakitaka Hakimu apigwe
kutokana na kinachodaiwa kuwa kajijengea mazingira ya rushwa.
Baada ya kuamuliwa hakimu huyo alimfuata tena Bwana Kilindu na kumkunja mbele ya Kituo
cha Polisi cha Iyula,Wilayani Mbozi huku akiporomosha matusi ya nguoni
na kushangaza wananchi baada ya kuzivunja sheria ili hali kapewa
dhamana ya kuzisimamia.
Aidha,kesi
hiyo iliyokuwa ikimhusisha Bwana Laurence ambaye amehukumiwa kwenda
jela miaka mitatu na baadae kukata rufaa katika Mahakama ya wilaya ya
Mbozi na kuachiwa huru lakini alibambikiziwa kesi nyingine akidaiwa
kuwapiga wananchi watatu wanaoishia katika Kijiji cha Ichesa wilayani
humo.
Mtuhumiwa
Laurence amekuwepo jela kwa muda wa mwezi mmoja,ambapo ndugu na jamaa
walifika siku ya Jumatatu Julai 23 mwaka huu kwa ajili ya kuomba
kumwekea dhamana ambapo Hakimu huyo Bi.Kivelege alikataa na kuwataka
wafike siku inayofuata Julai 24 wakiwa na barua ya udhamini.
Aidha,walipofika
siku hiyo Julai 24 mwaka huu wakiwa na barua ya udhamini,bado
hakuwasikiliza hadi ilipofika majira ya saa 9:30 alasiri ndipo alipotoa
hati ya kumtoa gerezani na mshitakiwa kufikishwa Kituo cha Polisi cha
Iyula majira ya saa 12:30 jioni na kudhaminiwa na kaka yake mbele ya
Mkuu wa kituo hicho Mkaguzi msaidizi Inspekta Uziweli Mwanga ambapo
alitakiwa kufika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili.
Julai
25 mwaka huu mshitakiwa alifika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza
kesi inayomkabili lakini kabla ya kesi Bwana Laurence Julias
aliwasilisha barua yenye sababu ya kumpinga hakimu huyo,ambapo sababu
ya kwanza akidai hana imani naye, ya pili yupo karibu na walalamikaji
na mwisho alidai kwamba kesi yake aliomba kutosikilizwa na hakimu huyo
ambaye alitoa hukumu ya kwenda jela miaka mitatu bila sababu ya msingi.
Kufuatia
hali hiyo Hakimu Bi Kivelege alionekana kukasirishwa na barua
hiyo,hivyo kumtaka mshitakiwa adhaminiwe upya na kumamuru Mkuu wa Kituo
cha polisi kumweka mahabusu hali iliyowakasirisha ndugu zake na kuleta
tafrani kubwa katika kituo hicho.
Hata
hivyo baada ya kuona hali hiyo Mkuu wa kituo hicho cha Polisi Inspekta
Mwanga alimrejesha Bwana Laurence mahakamani ndipo zogo
lililopoanza,hakimu akitaka dhamana ya awali ifutwe huku sababu za
kufutwa hazikuwekwa bayana.
Wakati huohuo Hakimu hakuendelea na kesi huku akiondoka na gari yake akiacha kesi nyingine bila kusikilizwa lakini katika
uchunguzi uliofanya ulibaini kuwa jumla ya kesi 9 zilizohukumiwa na
hakimu huyo zimekatiwa rufaa kutokana na watuhumiwa kuachiwa huru
mahakama ya wilaya hali inayotia shaka utendaji kazi wake.
SOURCE http://chimbukoletu.blogspot.com
No comments:
Post a Comment