Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, August 15, 2012

MASHINDANO YA BANCABC SUPER8 SIMBA VS AZAM NUSU FAINALI LEO KATIKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR



Katikati ni Mkurugenzi mtendaji wa bank ABC Boniphace Nyoni na kushoto kwake ni Mkurugenzi mkuu wa kitengo cha fedha Mwalim Zuberi na kulia kwake ni kocha wa Timu ya Jamhuri Ameri Chuwa.
 Kocha wa timu ya Mtibwa Sugar Mecky wakati akiongea na waandishi wa habari.

Nusu fainali zitapigwa Uwanja wa Taifa kesho Jumatano, ambako Simbaa itavaana na Azam huku Mtibwa sugar ikipepetana na Jamhuri. Mchezo wa kwanza utaanza saa nane mchana wataanza Mtibwa sugar na Jamhuri ya Zanzibar na mchezo wa pili ni kati ya Simba Vs Azam utakao anza saa kumi.
 
  
MTIBWA, Simba, Azam FC na Jamhuri ya Pemba zimefanikiwa kupenya hatua ya nusu fainali ya michuano ya BancABC SUP8R inayondelea katika vituo vinne hapa nchini.

Michuano hiyo inayodhaminiwa na Banc ABC, ilikuwa ikirindima katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Zanzibar na sasa imefikia hatua ya nusu fainali.

August 12 mwaka huu kwenye dimba la Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam, ilishuhudiwa kwa mara ya pili nyuki wakikatiza uwanjani hapo, Jamhuri iliichapa Mtende kwa mabao 4-0.

Mabao ya washindi yalifungwa na Sadik Rajab dakika ya 28 na 45, Selemani Nuhu dakika ya 82 huku Suleiman Ally akikandamiza la nne dakika ya 90.

Kwenye dimba la Kirumba Mwanza, makinda wa Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Zimamoto yote yakitiwa kimiani na Edward Christopher, wakati huko Moshi kwenye Uwanja wa Ushirika, Azam FC iliifunga Polisi Morogoro kwa mabao 2-1.

Bingwa katika michuano hiyo atajitwalia kombe na kitita cha sh milioni 40, wa pili milioni 20 huku timu zitakazoishia nusu fainali kila moja itapata sh mil 15 na zitakazosalia zitajipoza kwa sh milioni 5 kila moja.

No comments:

Post a Comment