Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, August 6, 2012

WAKATI NA ANDIKA YA MOYONI ,MACHOZI YALINITOKA ASEMA DOGO JANJA.


Dogo Janja amesema maisha yake toka amejiunga na Mtanashati yamebadilika sana na hajutii uamuzi huo.Dogo Janja wa sasa sio yule wa zamani sababu amebadilika sana .Amesema kwa sasa anaishi kama star pia anamuonekano wa star  na amejitambua anataka nini kwenye mziki na maisha . Mimi kama Dogo Janja nilikuwa star ila sikuwa naishi kama star ,Nilikuwa naishi kama msela ila kwa sasa nina furaha na maisha yangu .
Dogo Janja Wakati Wa Epic Nation Tour 2011
Hii ndio nyimbo yakwanza kutoa chini ya Mtanashati na niliandika wimbo huu nikiwa kwenye wakati mgumu sana , Mashairi ya wimbo huu niliandika nikiwa nalia sababu yote nayosema yalitoka moyoni na mengine wakati nakumbuka nilikuwa nalia sana . Mimi na PNC Tulijifungia ndani tu na ndio nikawa naadika hii ngoma .Wimbo huu ulinikumbusha machungu mengi ,Baada ya kumaliza kuandika nilimfata Marco Chali na akanipa mdundo mzuri wakufanyia vocal bila shaka wimbo unaeleweka . Kwenye nyimbo hii sijamuongelea mtu wala ku diss mtu yoyote so mashairi haya yasitafrisiwe vibaya .

1 comment:

  1. Big up Dog Janja. Ndo maisha hayo, na ndo kukomaa huko.

    ReplyDelete