Dogo
Janja amesema maisha yake toka amejiunga na Mtanashati yamebadilika
sana na hajutii uamuzi huo.Dogo Janja wa sasa sio yule wa zamani sababu
amebadilika sana .Amesema kwa sasa anaishi kama star pia anamuonekano wa
star na amejitambua anataka nini kwenye mziki na maisha . Mimi kama
Dogo Janja nilikuwa star ila sikuwa naishi kama star ,Nilikuwa naishi
kama msela ila kwa sasa nina furaha na maisha yangu .
|
Dogo Janja Wakati Wa Epic Nation Tour 2011 |
Hii
ndio nyimbo yakwanza kutoa chini ya Mtanashati na niliandika wimbo huu
nikiwa kwenye wakati mgumu sana , Mashairi ya wimbo huu niliandika
nikiwa nalia sababu yote nayosema yalitoka moyoni na mengine wakati
nakumbuka nilikuwa nalia sana . Mimi na PNC Tulijifungia ndani tu na
ndio nikawa naadika hii ngoma .Wimbo huu ulinikumbusha machungu mengi
,Baada ya kumaliza kuandika nilimfata Marco Chali na akanipa mdundo
mzuri wakufanyia vocal bila shaka wimbo unaeleweka . Kwenye nyimbo hii
sijamuongelea mtu wala ku diss mtu yoyote so mashairi haya yasitafrisiwe
vibaya .
Big up Dog Janja. Ndo maisha hayo, na ndo kukomaa huko.
ReplyDelete