Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, September 2, 2012

Dar Ya Wanamapinduzi: Je, Che Guevara Alilala Wapi Alipokuwa Dar?


Ndugu zangu, 
Nimepata kukisoma kitabu kiitwacho " The African Dream"- The diaries of the revolutionary war in the Congo. Ama hakika ni kitabu chenye maelezo yenye kusisimua, kufurahisha na kusikitisha juu ya mwanamapinduzi Che Gueavara na harakati zake za mapambano ya ukombozi wa kimataifa. Ni kweli kuwa Che aliingia Dar April 1965 na alikutana na Nyerere ili kupata baraka zake kabla ya kwenda Congo Mashariki.

Hata hivyo, katika kitabu hicho Che hakuweka wazi jina la hotel aliyoishi alipokuwa Dar. Lakini kwa Dar ilivyokuwa hata miaka ya 70 ambayo nami nina kumbukumbu ya kutosha kwa kuona, basi,kulikuwa na restaurants nne pale katikati ya jiji ambazo nami nimeziona kwa macho na nimepata kuingia mara kadhaa utotoni, nazo ni Zahir Restaurant ( Sasa New Zahir Restaurant iliyo Mtaa wa Msikiti). Ni Restaurant hii ambayo Che alikwenda mahali hapo kwa chakula na chai. Kulikuwa pia na Royal Restaurant na Nakhuda Restaurant zote zikiwa Mtaa wa Jamhuri. Restaurant ya nne iliitwa The Khalid pale mtaa wa Kipande.

Hitimisho. Kama Che Guevara alikunywa chai na kula chakula Zahir Restaurant,basi,yawezekana kabisa kuwa ama aliishi Zahir Guest House iliyokuwa nyuma ya mgahawa huo, au kwenye  Ubalozi wa Cuba pale Upanga. 

Na kwanini hilo halikuwekwa wazi katika kitabu cha kumbukumbu zake siwezi kujua,maana siamini kama aliishi kwenye moja ya hoteli za gharama jijini Dar kwa vile hakutaka hata kwenda New Africa Hotel ambapo ndio ilikuwa kijiwe cha akina Abeid Karume na wapigania ukombozi wengine. Ni kwa vile, Che Guevara hakutaka kabisa kuonekana na mawakala wa CIA. 

Maggid Mjengwa,
Iringa,
0788 111 765

No comments:

Post a Comment