Mkali mwenye hit kibao kila mwaka kila akitoa na sasa ana hit moja
kubwa sana inayokwenda kwa jina la mtoto wa kariakoo prince dully sykes
anatafutwa na majamaa yanayosemekana kuwa ni wanajeshi. tukio ilo
lilitokea juzi katika ukumbi wa mzalendo ambapo dully ilitokea kupishana
lugha na mjeda mmoja aliekuwa kavaa kiraia na hapo ndipo mjeda yule
akatishia kumtupa dully kutoka juu ya ghorofa hiyo ya mzalendo mpaka
chini, hapo ndipo dully alipomruhusu bounsa wake kufanya kazi yake
anaejulikana kwa jina la arafat ngumi jiwe. bunsa huyo kama kawaida yake
na jina lake lilivyo akamtwanga sana jamaa huyo bila yakujua kama ni
mjeda. akiongea na xdeejayz arafat ngumi jiwe amesema sisi tumeamua
kujihami kwani yule jamaaa alikuwa anataka kumtupa dully kutoka
ghorofani hivyo ndio tukajihami kwa kumpiga. akaulizwa" unajuakama
jamaa uliempiga ni mwanajeshi? akasema yeye ajui ni nani? chanzo chetu
cha habari kinasema dully sykes ameamua kujificha kutokana na salam
amnazozipata kama kuna wanajeshi wanakutafuta leo siku ya pili.
Dully sykes akiwa na baunsa wake Arafat ngumi jiwe
No comments:
Post a Comment