Siku
mbili baada ya kifo cha mwandishi mwenzao wa habari (Daudi Mwangosi)
aliefariki kutokana na kulipukiwa na bomu akiwa mikononi mwa polisi
waliokuwa wanatawanya wafuasi wa Chadema huko Iringa, mwandishi wa
habari Francis Godwin ambae alikua rafiki wa marehemu amejisalimisha
polisi kufata masharti ya taarifa iliyotolewa kwa yeye na wenzake wawili
kusakwa na polisi.
Exclusive
na millardayo.com namkariri Godwin akisema “kutokana na hali halisi ya
kushuhudia tukio la mauaji ya Mwangosi, nilifukuziwa kwa nyuma na gari
lisilokua na namba pia nilipofika nyumbani niliambiwa kuna watu walikuja
kuniulizia lakini hawafahamiki, na taarifa zikatoka kwamba tunasakwa”
Kuhusu
kujisalimisha, Godwin amesema aliamua kufanya huo uamuzi baada ya
kusikia taarifa za kusakwa kwake pamoja na waandishi wengine wawili,
jana (september 5) aliamua kujisalimisha mwenyewe Polisi akiwa
amesindikizwa na waandishi wa habari kama hamsini ambapo baada ya kufika
pale walikutana na kamishna wa makosa ya jinai Tanzania Robert Manumba
ambae ilibidi ahoji polisi Iringa kama ni kweli wanamtafuta Godwin na
wenzake.
Kingine
kilichoendelea baada ya hapo ni Club ya waandishi wa habari Iringa
kuziomba redio mbalimbali za iringa ambazo zimekua zikirusha matangazo
ya polisi jamii kusimamisha matangazo hayo ambapo wamiliki wa vyombo
hivyo wamekubali ombi.Namkariri
Godwin akisema “baada ya kumuuliza mmoja kati ya maofisa wake kama ni
kweli wanamtafuta Godwin ofisa huyo alijiumauma na baadae akasema
hatumtafuti, baada ya hapo waandishi wa habari tulisimama tukaondoka kwa
sababu ya kutokubaliana na kilichotaka kuendelea kuhusu taarifa ya
uchunguzi ya Manumba”
Francis
Godwin ambae alikua karibu na marehemu Daudi Mwangosi muda mfupi kabla
ya kuuwawa kwa bomu amesema “Nilijua kwamba mimi ni miongoni mwa
waandishi watatu wanaotafutwa kwa sababu marehemu kabla ya kifo akiwa
amekamatwa nilitaka kwenda kumuokoa pale lakini nilipokua namsogelea
Daudi akaniambia Godwin mdogo wangu kimbia… wakati nakimbia kama hatua
20 mbele nyuma nageuka nasikia mlipuko mkubwa, kuangalia ni Wangosi
amekufa na nilibahatika kupiga baadhi ya picha ambapo askari waliokuwepo
walipoona narudi kwenye eneo hilo walinionyeshea bunduki ikabidi
ninyooshe mikono juu kwamba jamani mimi nakuja kwa heri wakaniambia
potea”
Godwin
amesema baada ya kugeuka na kuanza kukimbia walianza kumfukuzia ila
bahati nzuri gari yake ilikua mbali, baada ya kutishwa na polisi
walipokwenda hospitali ulipopelekwa mwili wa marehemu ilibidi waanze
kutoa mabango ya wanahabari yaliyobandikwa kwenye gari yao pamoja na
kutoa namba za gari, alianza safari ya kuondoka lakini kuna gari zilikua
zinamfukuzia kwa nyuma mpaka alipofika nje kidogo ya mji wa Iringa na
kuingia mitaani ndio akafanikiwa kukimbia.
Kwenye
sentensi ya mwisho Godwin anasema ameibiwa siri na askari mmoja ambae
alimwambia kuhusu kutafutwa kwake yeye na waandishi wa habari awengine
mbapo alimuonya kwamba msimamo na kauli aliokua ameutoa pamoja na
ushahidi wa tukio la mauaji ndio vimefanya atafutwe
source milladayo
No comments:
Post a Comment