Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa Tuzo ya Uongozi Bora wa sera ya
Kilimo na Chakula toka kwa Bw. Ajay VAshee, Makamu Mwenyekiti wa asasi
isiyo ya kiserikali inayohusika na sera za kilimo na chakula na
Maliasili n ijulikanayo kama Food, Agriculture and Natural Resources
Policy (FANRPAN) katika hoteli ya White Sands jana Septemba 5, 2012.
Anayeshuhudia kulia ni Katibu Mtendaji wa FANRPAN) Dkt Lindiwe Sibanda.
Tuzo hiyo, ambayo hutolewa kwa kiongozi aliyefanya juhudi kuhakikisha
kuwepo kwa sera bora za kilimo na chakula nchini kwake, ilichukuliwa na
Malkia Ntombi Indlovukazi wa Swaziland mwaka jana, wakati Rais
Hifikepunye Pohamba alitunukiwa mwaka 2010, Rais Armando Emilio Gwebuza
mwaka 2009 na Rais wa Malawi, Hayati Bingu Wa Mutharika, aliipokea
mwaka 2008.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia baadhi ya ng'ombe anaowafuga kwa
kufuata njia za kisasa kwenye shamba lake kijijini kwake Msoga,
Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, leo Septemba 6, 2012.PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment