WATU
saba wamepoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo ya
madini yaliyopo katika kata ya Nandagala wilayani ya Ruangwa mkoani
Lindi.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hii Diwani wa kata hiyo, Andrew
Chikongwe alisema kuwa kazi ya kufukua kifusi na kutoa miili ya marehemu
hayo ilianza majira ya saa 9 alasiri hadi mapema asubuhi huku
wakifanikiwa kupata miili yote.
Chikongwe
alisema kuwa kazi hiyo ilikuwa ngumu kutokana na kuwepo kwa zana duni
za uokoaji wakati wa kufukua mchanga na hatimaye kupata miili hiyo.
Diwani
huyo aliwataja marehemu hao kuwa ni Nyang'ana Mkelecha mkazi wa Musoma,
Mohamed Omari Fondogoro Mkazi wa Morogoro, Bakari Liganga mkazi wa
Chunyu Ruangwa.
Wengine
ni Rajab maarufu ROGER mkazi wa Musoma, Uwesu Bakari Abeid mkazi wa
Rondo ,Chakoda mkazi wa Dar na Rashid Ally maarufu BADE mkazi wa Masasi
mkoani Mtwara.
source issa michuzi
No comments:
Post a Comment