Pages

Thursday, September 6, 2012

SIMBA YAPIGWAA GOLI TATU BILA NA SOFAPAK


11 walioanza leo

Mrisho Ngassa akiwatoka mabeki wa Sofapaka

Mwinyi Kazimoto akijiandaa kutia krosi

George Owino akimdhibiti Salim Kinje

Haruna Moshi kulia akizungumza na George Owino wakati Akuffo ameumia anapatiwa huduma ya kwanza kabla ya kutolewa

Edward Chiristopher akitafuta mbinu za kumtoka Edgar Ochieng

Edward Chirstopher Edward akimtoka Edgar Ochieng
IMEANDIKWA NA BONGOSTAZ
SIMBA imeshindwa kuwafurahisha mashabiki wake jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya kufungwa mabao 3-0 na Sofapaka ya Kenya katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC Jumanne ijayo kwenye Uwanja huo huo.
Hadi mapumziko, Sofapaka walikuwa kwa bao 1-0, lililofungwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, John Barasa kwa penalti dakika ya 19, akiupeleka mpira kulia na Juma Kaseja akichupa kushoto upande wa kushoto.
Penalti hiyo ilitolewa baada ya Komabil Keita kuunawa mpira kwenye eneo la hatari wakati akiwa katika jitihada za kuokoa hatari langoni mwake.
Mshambuliaji Danniel Akuffo alitolewa nje dakika ya 40 baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Abdallah Juma. 
Kipindi cha pili, Sofapaka walirudi na moto tena na kufanikiwa bao la pili dakika ya 55 mfungaji Barasa tena kabla ya Joseph Nyaga kufunga la tatu dakika ya 66.
Kwa nini Simba wamefungwa? Walizidiwa uwezo na Sofapaka, ambao walicheza kwa kuelewana zaidi tangu mwanzo wa mchezo.
Simba SC; Juma Kaseja (1), Shomary Kapombe (15), Amir Maftah (17)/Paul Ngalema, Paschal Ochieng (5), Komabil Keita (4)/Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto (14), Salim Kinje/Ramadhani Chombo (12)/, Haruna Moshi (3)/Kiggi Makassy, Edward Christopher (19)/Nassor Masoud, Daniel Akuffo (13)/Abdallah Juma na Mrisho Ngassa (16).
Kocha; Profesa Milovan Cirkovick (Serbia)
Sofapaka FC; Duncan Ochieng (39), Anthony Kimani (11), James Situma (14), Edgar Ochieng (5), George Owino (26), Collins Okoth (45), Osborne Monday (2)/Thomas Wanyama, Danson Kago (13)/Hashimu Mukwana, Joseph Nyangit (30), Humphrey Mieno (20)/Robert Binja na John Baraza (19).
Kocha; David Ouma (Kenya)

No comments:

Post a Comment