|
11 walioanza leo |
|
Mrisho Ngassa akiwatoka mabeki wa Sofapaka |
|
Mwinyi Kazimoto akijiandaa kutia krosi |
|
George Owino akimdhibiti Salim Kinje |
|
Haruna Moshi kulia akizungumza na George Owino wakati Akuffo ameumia anapatiwa huduma ya kwanza kabla ya kutolewa |
|
Edward Chiristopher akitafuta mbinu za kumtoka Edgar Ochieng |
|
Edward Chirstopher Edward akimtoka Edgar Ochieng |
IMEANDIKWA NA BONGOSTAZ
SIMBA
imeshindwa kuwafurahisha mashabiki wake jioni hii kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam baada ya kufungwa mabao 3-0 na Sofapaka ya Kenya
katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi
ya Azam FC Jumanne ijayo kwenye Uwanja huo huo.
Hadi
mapumziko, Sofapaka walikuwa kwa bao 1-0, lililofungwa na mshambuliaji
wa zamani wa Yanga, John Barasa kwa penalti dakika ya 19, akiupeleka
mpira kulia na Juma Kaseja akichupa kushoto upande wa kushoto.
Penalti
hiyo ilitolewa baada ya Komabil Keita kuunawa mpira kwenye eneo la
hatari wakati akiwa katika jitihada za kuokoa hatari langoni mwake.
Mshambuliaji Danniel Akuffo alitolewa nje dakika ya 40 baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Abdallah Juma.
Kipindi
cha pili, Sofapaka walirudi na moto tena na kufanikiwa bao la pili
dakika ya 55 mfungaji Barasa tena kabla ya Joseph Nyaga kufunga la tatu
dakika ya 66.
Kwa nini Simba wamefungwa? Walizidiwa uwezo na Sofapaka, ambao walicheza kwa kuelewana zaidi tangu mwanzo wa mchezo.
Simba SC;
Juma Kaseja (1), Shomary Kapombe (15), Amir Maftah (17)/Paul Ngalema,
Paschal Ochieng (5), Komabil Keita (4)/Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto
(14), Salim Kinje/Ramadhani Chombo (12)/, Haruna Moshi (3)/Kiggi
Makassy, Edward Christopher (19)/Nassor Masoud, Daniel Akuffo
(13)/Abdallah Juma na Mrisho Ngassa (16).
Kocha; Profesa Milovan Cirkovick (Serbia)
Sofapaka FC;
Duncan Ochieng (39), Anthony Kimani (11), James Situma (14), Edgar
Ochieng (5), George Owino (26), Collins Okoth (45), Osborne Monday
(2)/Thomas Wanyama, Danson Kago (13)/Hashimu Mukwana, Joseph Nyangit
(30), Humphrey Mieno (20)/Robert Binja na John Baraza (19).
Kocha; David Ouma (Kenya)
No comments:
Post a Comment