Azam FC |
Na Prince Akbar
LIGI Kuu ya soka
ya Vodacom Tanzania Bara leo inaingia katika raundi ya sita, kwa mechi mbili
kupigwa leo na nyingine tano kesho.
African Lyon
watakuwa wenyeji wa Azam katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Chamazi, au Azam
Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni.
Ruvu
Shooting wataikaribisha Coastal Union ya Tanga katika mechi itakayochezeshwa na
refa Oden Mbaga wa Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi
mkoani Pwani. Mbaga atasaidiwa na Samuel Mpenzu, Ferdinand Chacha na Andrew
Shamba.
Ligi hiyo
itaendelea kesho kwa mabingwa watetezi na vinara wa ligi hiyo, Simba kuumana na
Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam, wakati Kagera Sugar wataikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Kaitaba
mjini Bukoba.
Vibonde wa
ligi hiyo, Mgambo Shooting watakuwa wenyeji wa vibonde wengine wa ligi hiyo,
Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, wakati Toto Africans wataikaribisha
JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Kirumba mjini Mwanza na Tanzania Prisons watakuwa
wenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Azam inaweza
kupanda kileleni leo, iwapo itapata ushindi wa wastani mzuri wa mabao, kwani
itatimiza pointi 13 sawa na Simba na mabao ndiyo yataibeba juu ya Wekundu wa
Msimbazi.
Hadi sasa,
mwenendo wa ligi unaonyesha ushindani ni kati ya mabingwa watetezi, Simba SC na
washindi wa pili wa msimu uliopita, Azam FC ambazo zinakabana kileleni.
Hali bado si
nzuri kwa mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo, Yanga SC ambayo inazidiwa pointi
tano na mabingwa watetezi, Simba SC ambao pia ni wapinzani wao wa jadi.
Timu mbili
kati ya tatu zilizopanda Ligi Kuu msimu huu JKT Mgambo na Polisi Morogoro ndizo
zipo mkiani, wakati Prisons ndio inaonekana kuwa imara zaidi, kwani ipo nafasi
ya tano katika msimamo huo.
P W D L GF GA GD Pts
Simba SC 5 4 1 0 10 3 7 13
Azam FC 4 3 1 0 6 1 5 10
Coastal 5 2 2 0 7 5 2 8
Yanga SC 5 2 2 1 8 6 2 8
Prisons 5 2 2 1 6 5 1 8
Mtibwa Sugar 4 2 1 1 6 3 3 7
JKT Oljoro 4 1 3 1 4 3 1 6
African Lyon 5 2 0 3 5 9 -4 6
JKT Ruvu 5 2 0 3 4 10 -6 6
Kagera Sugar4 1 1 2 4 4 0 4
Toto African 4 0 3 1 4 4 0 3
Ruvu Shooting 5 1 0 4 6 10 -4 3
Polisi Moro 4 0 2 2 1 3 -2 2
JKT Mgambo 4 0 0 4 1 4 -3 0source http://bongostaz.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment