Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, October 6, 2012

KESI YA LULU:::::JOPO LA MAJAJI WARUDISHA JALADA LA KESI YA LULU MAKAHAMA YA KISUTU





MSANII WA LUNIGA LULU LEO KESI YAKE IMETUPILIWA MBALI AMBAYO ILIKUWA KWA AJILI TAMKO LAKE LA KUDAI UMRI WAKE NI MDOGO AMBAYO KESI YAKE ILIKUWA KATIKA MAHAKAMA KUU NA IMERUDISHWA TENA KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU KUSILIZWA TENA

MAHAKAMA ya Rufani Tanzania, imetengua uamuzi wa Jaji Dk. Fauz Twaib wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, wa kukubali kuufanyia uchunguzi umri wa msanii Elizabeth Michael 'Lulu'.
Uamuzi huo wa kuamuru kurudishwa kwa jalada la kesi ya msingi ya mauaji inayomkabili msanii machachari wa filamu nchini Elizabeth Michael (18), ‘Lulu’, kurudishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kuendelea na mwenendo wa shauri hilo.
Uamuzi huo ulitolewa leo na jopo la majaji watatu waliokuwa wakisikiliza maombi ya rufani hiyo wakiwa chini ya Mwenyekiti Jaji January Msoffe huku Majaji wengine walioketi kusikiliza maombi hayo ni Jaji Bernard Luanda na Jaji Edwin Rutakangwa
Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliwasilisha maombi Mahakama ya Rufani akitaka uamuzi wa Jaji Fauz alioutoa Juni 11, mwaka huu urejewe.
Lulu anatuhumiwa kwa kesi ya mauaji ya aliyekuwa msanii nyota nchini wa filamu marehemu msanii Steven Kanumba,aliyefariki dunia Aprili 7 mwaka huu nyumbani kwake maeno ya Vatican City , Sinza Jijini Dar es Salaam
Suala la umri wa Lulu lilizua utata baada ya msanii huyo kusomewa shitaka hilo, ambapo upande wa Jamhuri ulidai ana umri wa miaka 18, huku mawakili wake wakidai ana miaka 17.
Mawakili wanaomtetea Lulu ni Kennedy Fungamtama, Flugence Massawe na Peter Kibatala, waliomba mahakama ya Kisutu, mbele ya Hakimu Agustina Mbando, kuufanyia uchunguzi umri wa Lulu na kuomba ashitakiwe katika Mahakamama ya watoto na kupewa haki haki kama mtoto.
Hakimu huyo alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kufanya hivyo.
Kutokana na hilo, mawakili hao waliamua kuwasilisha maombi Mahakama Kuu, ambayo yalipangwa mbele ya Jaji Twaib Fauz aliyeamua kwa mamlaka aliyonayo kufanyia uchunguzi umri huo, licha ya maombi hayo kuwasilishwa yakiwa na kasoro kisheria.
Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Zahra Maruma, akisoma uamuzi kwa niaba ya jopo la majaji, alisema uwasilishwaji maombi ulikuwa na kasoro, hata hivyo, liliamua kulisikiliza kutokana na uzito wa kesi hiyo.
Alisema Jaji Twaib Fauz alikosea kwa kutumia vifungu ambavyo havimpi mamlaka ya kuufanyia uchunguzi umri wa Lulu.
"Kama uamuzi wa Jaji Fauz usingekuwa na dosari, maombi haya yangetupwa lakini kutokana na kuona dosari hizo ndiyo maana tunaamua kutoa maelekezo kwamba jalada lirudishwe Kisutu kuendelea na mwenendo wa kesi ya msingi," alisema Zahra akisoma uamuzi wa jopo hilo.
Majaji hao walisema Jaji Fauz hakutakiwa kuufanyia uchunguzi umri huo, bali alipaswa kurejesha jalada Mahakama ya Kisutu na kutoa maelekezo.
Kesi ya msingi ya Lulu inatajwa Mahakama ya Kisutu Oktoba 8 Jumatatu ijayo.

No comments:

Post a Comment