Pages

Saturday, October 6, 2012

AZAM FC KUPAA KILELENI LIGI KUU LEO?


Azam FC

Na Prince Akbar
LIGI Kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara leo inaingia katika raundi ya sita, kwa mechi mbili kupigwa leo na nyingine tano kesho.
African Lyon watakuwa wenyeji wa Azam katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Chamazi, au Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni.
Ruvu Shooting wataikaribisha Coastal Union ya Tanga katika mechi itakayochezeshwa na refa Oden Mbaga wa Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani. Mbaga atasaidiwa na Samuel Mpenzu, Ferdinand Chacha na Andrew Shamba.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mabingwa watetezi na vinara wa ligi hiyo, Simba kuumana na Oljoro JKT kwenye  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati Kagera Sugar wataikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Vibonde wa ligi hiyo, Mgambo Shooting watakuwa wenyeji wa vibonde wengine wa ligi hiyo, Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, wakati Toto Africans wataikaribisha JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Kirumba mjini Mwanza na Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Azam inaweza kupanda kileleni leo, iwapo itapata ushindi wa wastani mzuri wa mabao, kwani itatimiza pointi 13 sawa na Simba na mabao ndiyo yataibeba juu ya Wekundu wa Msimbazi.
Hadi sasa, mwenendo wa ligi unaonyesha ushindani ni kati ya mabingwa watetezi, Simba SC na washindi wa pili wa msimu uliopita, Azam FC ambazo zinakabana kileleni.
Hali bado si nzuri kwa mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo, Yanga SC ambayo inazidiwa pointi tano na mabingwa watetezi, Simba SC ambao pia ni wapinzani wao wa jadi.
Timu mbili kati ya tatu zilizopanda Ligi Kuu msimu huu JKT Mgambo na Polisi Morogoro ndizo zipo mkiani, wakati Prisons ndio inaonekana kuwa imara zaidi, kwani ipo nafasi ya tano katika msimamo huo.
P       W       D       L        GF     GA     GD     Pts
Simba SC             5          4          1          0          10       3          7          13
Azam FC             4          3          1          0          6          1          5          10
Coastal             5          2          2          0          7          5          2          8
Yanga SC           5          2          2          1          8          6          2          8
Prisons              5          2          2          1          6          5          1          8
Mtibwa Sugar 4          2          1          1          6          3          3          7
JKT Oljoro        4          1          3          1          4          3          1          6
African Lyon   5          2          0          3          5          9          -4        6
JKT Ruvu            5          2          0          3          4          10       -6        6
Kagera Sugar4         1          1          2          4          4          0          4
Toto African   4          0          3          1          4          4          0          3
Ruvu Shooting 5          1          0          4          6          10       -4        3
Polisi Moro       4          0          2          2          1          3          -2        2
JKT Mgambo     4          0          0          4          1          4          -3        0
source http://bongostaz.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment