MSANII
WA LUNIGA LULU LEO KESI YAKE IMETUPILIWA MBALI AMBAYO ILIKUWA KWA AJILI
TAMKO LAKE LA KUDAI UMRI WAKE NI MDOGO AMBAYO KESI YAKE ILIKUWA KATIKA
MAHAKAMA KUU NA IMERUDISHWA TENA KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU KUSILIZWA
TENA
MAHAKAMA
ya Rufani Tanzania, imetengua uamuzi wa Jaji Dk. Fauz Twaib wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, wa kukubali kuufanyia
uchunguzi umri wa msanii Elizabeth Michael 'Lulu'.
Uamuzi
huo wa kuamuru kurudishwa kwa jalada la kesi ya msingi ya mauaji
inayomkabili msanii machachari wa filamu nchini Elizabeth Michael (18),
‘Lulu’, kurudishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kuendelea na
mwenendo wa shauri hilo.
Uamuzi
huo ulitolewa leo na jopo la majaji watatu waliokuwa wakisikiliza
maombi ya rufani hiyo wakiwa chini ya Mwenyekiti Jaji January Msoffe
huku Majaji wengine walioketi kusikiliza maombi hayo ni Jaji Bernard
Luanda na Jaji Edwin Rutakangwa
Naye
Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliwasilisha maombi Mahakama ya Rufani
akitaka uamuzi wa Jaji Fauz alioutoa Juni 11, mwaka huu urejewe.
Lulu
anatuhumiwa kwa kesi ya mauaji ya aliyekuwa msanii nyota nchini wa
filamu marehemu msanii Steven Kanumba,aliyefariki dunia Aprili 7 mwaka
huu nyumbani kwake maeno ya Vatican City , Sinza Jijini Dar es Salaam
Suala
la umri wa Lulu lilizua utata baada ya msanii huyo kusomewa shitaka
hilo, ambapo upande wa Jamhuri ulidai ana umri wa miaka 18, huku
mawakili wake wakidai ana miaka 17.
Mawakili
wanaomtetea Lulu ni Kennedy Fungamtama, Flugence Massawe na Peter
Kibatala, waliomba mahakama ya Kisutu, mbele ya Hakimu Agustina Mbando,
kuufanyia uchunguzi umri wa Lulu na kuomba ashitakiwe katika Mahakamama
ya watoto na kupewa haki haki kama mtoto.
Hakimu huyo alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kufanya hivyo.
Kutokana
na hilo, mawakili hao waliamua kuwasilisha maombi Mahakama Kuu, ambayo
yalipangwa mbele ya Jaji Twaib Fauz aliyeamua kwa mamlaka aliyonayo
kufanyia uchunguzi umri huo, licha ya maombi hayo kuwasilishwa yakiwa na
kasoro kisheria.
Naibu
Msajili wa Mahakama ya Rufani, Zahra Maruma, akisoma uamuzi kwa niaba
ya jopo la majaji, alisema uwasilishwaji maombi ulikuwa na kasoro, hata
hivyo, liliamua kulisikiliza kutokana na uzito wa kesi hiyo.
Alisema Jaji Twaib Fauz alikosea kwa kutumia vifungu ambavyo havimpi mamlaka ya kuufanyia uchunguzi umri wa Lulu.
"Kama
uamuzi wa Jaji Fauz usingekuwa na dosari, maombi haya yangetupwa lakini
kutokana na kuona dosari hizo ndiyo maana tunaamua kutoa maelekezo
kwamba jalada lirudishwe Kisutu kuendelea na mwenendo wa kesi ya
msingi," alisema Zahra akisoma uamuzi wa jopo hilo.
Majaji
hao walisema Jaji Fauz hakutakiwa kuufanyia uchunguzi umri huo, bali
alipaswa kurejesha jalada Mahakama ya Kisutu na kutoa maelekezo.
Kesi ya msingi ya Lulu inatajwa Mahakama ya Kisutu Oktoba 8 Jumatatu ijayo.
No comments:
Post a Comment