Jared Loughner amehukumiwa kwa mauwaji ya watu sita ambaye pia alimjeruhi vibaya Mbunge katika bunge la Marekani Bibi Gabrielle Giffords katika tukio alilolifanya mwezi Januari mwaka jana. amehukumiwa vifungo saba vya maisha pamoja na miaka 140 gerezani.
Mtuhumiwa huyo Jared Loughner mwenye umri wa miaka 24 amehukumiwa vifungo saba vya maisha pamoja na miaka 140 gerezani, hukumu hiyo ni baada ya kufikia makubaliano na waendesha mashitaka mwezi Agosti ambayo yalimnusuru na adhabu ya kifo.
 Amekiri kwenda katika eneo la maduka la Tucson, Arizona ambako watu walikuwa katika tukio moja akiwa na mpango wa kumuuwa Giffords. Shambulizi hilo lilimuacha katika hali mbaya Bibi Giffords kwa kumjeruhi kichwani, kumsababishia ashindwe kuongea, kupooza mkono wa kulia pamoja na kupoteza uwezo wa kuona vizuri. Giffords alikuwepo mahakamani wakati hukumu hiyo inatolewa.