Brigedia general Hassan Ngilizi mwenekiti aliyekuwa anaongoza uchunguzi..
Spika wa Bunge Anna Makinda Wakati akisoma taarifa hiyo leo Bungeni Mjini Dodoma..
Mh sara Msafiri aliyekuwa anatuhumiwa.Amekutwa hana hatia katika ripoti hiyo..
Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka alituhumiwa lakini nae hana hatia.
Mh Maswi Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Amepewa Onyo kali na spika wa Bunge la tanzania..
Waziri wa
Nishati na Madini Mh Profesa Sospeter Muhongo nayea ameagizwa kuwa
muangalifu katika hotuba zake kwa kuwa ni muwakilishi wa serikali..
Mh Tundu
Lisu ambaye aliongea na waandishi wa habari na kuwatuhumu baadhi ya
bunge naye amepewa onyo kali na spika wa bunge la tanzania..
Mheshimiwa
John Mnyika mbunge wa ubungo na msemaji wa kambi ya upinzani bungeni
ambaye nae katika hotuba yake aliwatuhumu baadhi ya wabunge nae amepewa
onyo kali..
Mh
selasini mbunge wa Rombo nae alisimama bungeni wakati akichangia hoja ya
bugeti ya nishati na madina nae amepewa onyo kali na spika wa bunge la
tanzania..
Sehemu ya taarifa hiyo...
Maswi
aliwatuhumu moja kwa moja baadhi ya wabunge kwa maandishi kutaka rushwa
na wakimtishia kupoteza nafasi yake ya Ukatibu wa Wizara
- Tume inasema Maswi alitoa tuhuma hizi kwa lengo la kujihami juu ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili
- Tuhuma za kuwa Maswi aliombwa rushwa ya Milioni 50 na wabunge nazo zimetupiliwa mbali kuwa lengo ni kutaka kujihami.
- Mbunge Selasini alipohojiwa na Tume, alikiri kuwa hakuwa na ushahidi
wa maneno 'aliyoropoka' bungeni akiwatuhumu baadhi ya wabunge
waliohisiwa kupokea rushwa.
- Mnyika
alipohojiwa juu ya kauli yake Bungeni kuwa Maswi anashinikizwa ajiuzulu
nafasi yake, Mnyikaalitumia ushahidi wa vyombo mbalimbali vya habari!
Anadai kuwa hakukuwa na kanusho la habari hizo (labda ndilo lilimpelekea
kuamini ni habari sahihi)
- Ole Sendeka alipohojiwa juu ya kauli yake bungeni; alidai kuwa alikuwa anajaribu ku pre-empty tu.
- Mbunge Kessy naye alijikanyaga tu kuwa lazima kulikuwa na rushwa tu
- Waziri Muhongo alipohojiwa na Tume alisema ni 'allegations' tu.
- Mbunge Sarah Msafiri na mwenzake wamesafishwa, hawakuiuzia TANESCO
matairi! Tuhuma za Tundu Lissu pia zimeonekana kukosa mashiko na amekiri
kuwa alipata taarifa toka kwa watu wa Wizara, hakuwa na ushahidi
wa moja kwa moja!
- Wabunge waliotoa tuhuma bungeni, wamekemewa na kutakiwa kutorudia tena.
- Lissu amekaripiwa vikali kwa kuwachafua wabunge na waliochafuliwa wameombwa wamsamehe bure.
- Waziri Sospeter Muhongo amekaripiwa kwa kuwachafua wabunge na
ametakiwa awe mwangalifu anapotoa kauli yoyote bungeni kwakuwa kauli
yake inachukuliwa ni kauli ya Serikali.
No comments:
Post a Comment