Pages

Thursday, November 29, 2012

FERGUSON AITOA CHELSEA MBIO ZA UBINGWA WA ENGLAND




MANCHESTER, England

“Matokeo ya leo usiku yanatuweka sisi mbali kidogo na Chelsea  
katika mbio za ubingwa wa ligi. Sisi bado tuko mbele tukiongoza 
msimamo wa ligi, lakini Man City wako karibu yetu na msimu bado ni mrefu”

KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amekenulia meno
 mwanzo mbaya wa kocha wa Chelsea, Rafa Benitez klabuni
 Stamford Bridge, na kutabiri ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu 
ni kinyang’anyiro cha timu za jiji la Manchester.

Chelsea inayoshikilia ubingwa wa soka barani Ulaya, iko nyuma
 kwa pointi saba nyuma ya vinara Man United na sita, nyuma ya
 mabingwa watetezi Man City.

Fergie bosi wa Man United, alisema: “Matokeo ya leo usiku 
yanatuweka sisi mbali kidogo na Chelsea katika mbio za ubingwa wa ligi.

“Sisi bado tuko mbele tukiongoza msimamo wa ligi, lakini
 Man City wako karibu yetu na msimu bado ni mrefu.

“Umuhimu wa kushinda bao 1-0 katika baadhi ya mechi, 
unawaonesha wapinzani wako kiasi cha ujasiri mlichonacho.

“Kama utaangalia baadhi ya mechi muhimu za matokeo ya bao
 1-0 tuliowahi kupata... rejea nyuma kabisa tulipoicaha Newcastle
 wakati wakiwa pointi tisa juu yetu mwaka 1996 – ushindi wetu wa 
1-0 usiku huo, ukatuwezesha kutupa ubingwa.

“Kulikuwa na umuhimu wa ushindi wa 1-0. tulifanya hivyo kwa wengi wao.”

No comments:

Post a Comment