Novemba 15, mwaka huu mapadri hao ambao
wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa wakiendelea na matibabu, walivamia
na kushambuliwa kwa silaha za moto, mapanga na nondo na majambazi.
Watu watano wanaosikiliwa na polisi
wakihusishwa na uhalifu huo katika tukio hilo ambalo mapadri hao mbali na
kujeruhiwa vibaya waliibiwa zaidi ya sh Milioni 3.8.
Akiwasilisha salamu za Rais, Lukuvi alisema
ametumwa kutoa pole kwa wahanga hao, waumini na viongozi wa dhehebu hilo la dini
kwa ujumla wake.
“Tupo pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu
ambacho majambazi wamekuwa wakiwavamia viongozi wa dhehebu hili la dini
wakiamini mmehifadhi fedha na mali nyingine nyingi ndani ya parokia zenu,”
alisema.
Alisema tukio la mapadri hao kuvamiwa na
kujeruhiwa mkoani Iringa limekuja miezi michache baada ya matukio kama hayo
kutokea katika parokia za Migori na Pawaga mkoani Iringa.
“Serikali imefanya kazi ya kutoa mafunzo kwa
mgambo wengi karibu katika kila kijiji, ni wajibu wa taasisi hizi za dini
kuwatumia hao au vinginevyo ikubali kushirikiana na jeshi la Polisi kutoa
mafunzo kwa walinzi wao,” alisema.
Akipokea salamu hizo, Padro Burgeo alisema
majambazi hao walifanikiwa kuingia ndani ya parokia yake baada ya kutumia lango
la nyuma na kufanikiwa kuwapiga chenga walinzi wao.
Alisema katika tukio hilo ilikuwa afe lakini
Mungu amesaidia kuyanusuru maisha yake baada ya kufikishwa mikononi mwa
madaktari.
Kaimu wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dk Faustine
Gwanchele alisema baada ya kumfanyia upasuaji na kutoa risasi tatu kwa Padri
Burgeo hali yake inaendelea vizuri pamoja na kusumbuliwa na ugonjwa wa
kisukari
No comments:
Post a Comment