Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA David Petraeus (pichani) amejiuzulu nafasi hiyo.
Katika taarifa yake kwa maafisa wa CIA, Mkuu huyo wa Iidara  ya Upepelezi wa Marekani amekiri kuwa na mahusiano nje ya ndoa yake, na kukielezea kitendo chake hicho kama kisichokubalika kwa kiongozi wa upelelezi.
Katika tamko lake Rais Barack Obama wa Marekani amesema kuwa amakebali kujiuzulu huko na kusema kuwa Petraeus ni mmoja kati ya maafisa bora wakuu wa kizazi hiki.