Nyumba ya Waziri wetu mstaafu na mbunge wetu Mstaafu Jackson Makweta.
Spika wa Bunge la TZ Anne Makinda Akitoa heshima za mwisho.
Askofu Japhet Mengele wa KKKT Dayosisi ya Njombe kUSINI Akiongoza misa wakati wa mazishi ya Hayati Jackson Makweta. WANAJESHI WA JWTZ WAKIWA WAMEBEBA MEZA KWA AJILI YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU
Askofu Japhet Mengele wa KKKT Dayosisi ya Njombe kUSINI Akiongoza misa wakati wa mazishi ya Hayati Jackson Makweta. WANAJESHI WA JWTZ WAKIWA WAMEBEBA MEZA KWA AJILI YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU
Waziri Wassira na jopo la waombolezaji wakiwa kwenye sala ya mwisho kumuaaga Jackson Makweta.
Mwili wa Hayati Jackson Makweta ukiagwa.
viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya ya Wanging'ombe Esterina Kilasi,Josephene Matiro DC Makete wakiwa msibani leo.
MKuu wa mkoa wa Njombe Capt.Mstaafu Asseri Msangi kushoto katikati ni Naibu waziri wa Ujenzi ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi Mhandisi Gerson Lwenge na kulia ni mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro wakiwa msibani Hagafilo Njombe leo hii.
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Mazishi ya aliyekuwa mbunge Mstaafu wa Jimbo la Njombe kaskazini Jakson Makweta yamefanyika leo nyumbani kwake Hagafilo Njombe yakisindikizwa naviongozi mbalimbali wa serikali kutoka mikoa mbalimbali hadi Taifani akiwemo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete na Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda.
Akizungumza kwenye mazishi ya marehemu Makweta kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa nchi ofisi ya Rais uhusiano na uratibu Steven Wassira amesema marehemu Makweta ameacha pengo kubwa kwa Taifa la Tanzania ambapo alikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha shule za NDDT zinaanzishwa pamoja na shule za sekondari za kata.
Aidha Waziri Wassira amesema Marehemu Makweta wakati wa uhai akiwa anaumwa aliweza kuacha wosia kwa viongozi waliokwenda kumutembelea kwa kusema razima viongozi wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wahakikishe kwamba ardhi ya watu wadogo haipokonywi wala kubadili matumizi ya ardhi yao kwa wakulima wadogo wa Tanzania.
Pia Waziri Wassira amesema kuwa Marehemu alisema serikali za mitaa zinafanya kazi nzuri sana lakini zinahitaji kusimamiwa na kumtaka Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kutoa mamlaka makubwa kwa wakuu wa mikoa Nnchini kusimamia serikali za mitaa ili maendeleo yaweze kufanikiwa .
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amesema marehemu Makweta alikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha shughuli za maendeleo zinasonga mbele ikiwemo kupigania mgawanyo wa mikoa mbalimbali hapa nchini pamoja na mkoa wa Njombe kugawanywa katika majimbo na wilaya zake.
Aidha Spika Makinda amesisitiza upendo katika jamii nakusema kuwa marehemu alikuwa na upendo kwa kila mmoja na kwa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutoa ushauri wa maendeleo ambapo kwa wale waliobahatika kupokea wosia wake wanapaswa kuuenzi na kuyafanyia kazi mawazo yake.
Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye amesema Marehemu Makweta ni mfano mzuri wa kuigwa na jamii kwa maatendo aliyoyafanya wakati wa uhai wake kwani marehemu aliweza kupambana na adui wawili Rushwa na Dhuruma katika jamii tatizo ambalo limeonekana kuwa sugu machoni pa jamii kwa maiasha ya sasa.
No comments:
Post a Comment