Pages

Wednesday, November 7, 2012

VIWANGO VYA UBORA VYA FIFA TANZANIA YASHUKA, BRAZIL HAIPO TOP 10




Katika Listi ya FIFA ya Ubora Duniani iliyotolewa leo, Mabingwa wa Dunia, Spain, bado wanashikilia Nambari Wani wakifuatiwa na Germany na Tanzania imeporomoka nafasi 2 na sasa ipo nafasi ya 134.
Argentina wameitoa Portugal kwenye nafasi ya 3 na wao kuikamata nafasi hiyo huku Russia wakiingia kwenye 10 Bora wakiwa nafasi ya 9 na Croatia wamepanda hadi nafasi ya 10.
Nchi ya Afrika ambayo ipo juu sana ni Ivory Coast iliyoshika nafasi ya 15 baada ya kupanda nafasi moja.
Brazil, ambao ndio Wenyeji wa Kombe la Dunia Mwaka 2014 na hivyo hawana Mechi za Mchujo kuingia Fainali hizo ambazo ndizo zinawakosesha Pointi za kupanda juu kwenye Ubora, wamebaki nafasi ya 13.
Listi nyingine ya FIFA ya Ubora Duniani itatolewa Mwezi ujao hapo Desemba 19.
20 BORA:
1 Spain
2 Germany
3 Argentina
4 Portugal
5 Italy
6 England
7 Netherlands
8 Colombia
9 Russia
10 Croatia
11 Uruguay
12 Greece
13 Brazil
14 Mexico
15 Côte d'Ivoire
16 Switzerland
17 Ecuador
18 France
19 Algeria
20 Belgium

No comments:

Post a Comment