Kocha Mkuu Ernest Brandts akiwa na mjumbe wa kamatai ya utendaji ambaye pia ni mkuu wa msafara Mohamed Nyenge
|
Ladislaus Mbogo akiwa na Nadir Haroub Canavaro Uwanja wa Ndege JK Nyerere — |
|
Viongozi wa Yanga wakiwa uwanja wa ndege |
YANGA
SC, mabingwa mara tano wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe
la Kagame wameondoka Alfajiri ya leo, saa 10:30 usiku kwenda Uturuki
kuweka kambi ya mazoezi ya wiki mbili.
Kikosi
kizima cha Yanga kilikuwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere tangu saa
8:00 usiku kwa taratibu za kusafiri katika ziara hiyo Yanga
itaweka kambi katika mji wa Antalya uliopo kusini mwa Uturuki na
itafikia katika hoteli ya Sueno Beach iliyopo pembezoni mwa bahari ya
Meditreanian, na itakua ikifanya mazoezi katika viwanja vikubwa viwili
vilivyopo katika hotel hiyo na kiwanja kidogo cha nyasi bandia.
Kikosi
cha Yanga kilichoondoka Alfajiri ya leo ni makipa; Ally Mustafa
'Barthez', Said Mohamed na Yussuf Abdul, mabeki Juma Abdul, Shadrack
Nsajigwa, Godfrey Taita, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua, Mbuyu Twite,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani.
Viungo
ni Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange
Twite, Nurdin Bakari, Omega Seme, Simon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar
Khalfani na David Luhende wakati washambuliaji ni Didier Kavumbagu, Said
Bahanunzi, Jerry Tegete, George Banda na Hamisi Kiiza.
Upande
wa benchi la ufundi ni Kocha Mkuu Mholanzi, Ernie Brandts, Kocha
Msaidizi Freddy Felix Minziro na Kocha wa makipa, Razak Ssiwa, na
Maofisa wengine ni Daktari wa timu, Sufiani Juma, Meneja Hafidh Saleh,
Ofisa Habari, Baraka Kizuguto Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mohammed
Nyenge.
Mwandishi
wa Gazeti la Mwanaspoti, Michael Momburi yupo kwenye ziara hiyo ya
kwanza ya Yanga Ulaya, yeye akigharamiwa na kampuni yake. |
No comments:
Post a Comment