Mbunge wa
jimbo la Ludewa na familia yake wakiwajulia hali wagonjwa kama
ilivyoutaratibu wake wa kila sikukuu kula na wagonjwa wa zanahati na
Hospitali mbalimbali jimboni mwake.
Mbunge Filikunjombe akitazama mikoni ya mtoto Diana ambayo imeungua kwa moto kushoto ni mama mzazi wa mtoto huyo
-----------------------
Mbunge
wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe, Deo Filikunjombe leo amejikuta
akibubujikwa na machozi baada ya kutembelea wodi la majeraha ya moto
katika Hositali ya Misheni Rugalawa na kukutana na mtoto Diana Haule
(11) mkazi wa Shaurimoyo ambaye ameungua kwa moto mwili wake na
kuimbiwa wimbo maalum uliomfanya kutokwa na machozi.
Mbunge huyo akiwa na familia yake ya mke na watoto wawili pamoja na viongozi wa CCM wilaya ya Ludewa aliofika katika wodi namba 6 ambapo mtoto huyo amelazwa, alipokelewa kwa wimbo maalum kutoka kwa mtoto huyo ambao ulikuwa ukimsifia Mbunge huyo.

Wakati
akiusikiliza na kumtazama mtoto huyo, Deo alianza kutokwa na machozi na
kulazimika kuwaomba watu ambao alikuwa ameongozana nao kutoka nje
ya chumba hicho na kumuacha yeye na mtoto huyo na watu wachache.
Katika wimbo huo mtoto huyo alikuwa akieleza jinsi ambavyo ameshindwa kuendelea na masomo kutokana na tatizo na ugonjwa wa kifafa linalomsumbua na pamoja na kumpongeza mbunge kwa kufika kumjulia hali.
Kutokana na maneno yawimbo huo, Mbunge Filikunjombe alijikuta akiinamisha kichwa chini na kuanza kutokwa na machozi huku akiendelea kumsikiliza mtoto huyo akiimba.
Hata hivyo, mbali na kueleza kusikitishwa na tatizo la Diana, bado mbunge huyo aliahidi kuendelea kumsaidia Diana, pamoja na kuisaidia Hospitali hiyo zaidi.
Mtoto huyo anadaiwa kuungua kwa moto toka mwezi wa tisa mwaka huu baada ya kuangukia motoni wakati akiwa na mama’ke mdogo jikoni akiendelea kuandaa chakula.
Wakati huo huo, Mhe. Filikunjombe amekabidhi misaada mbali mbali katika Hospitali hiyo yakiwemo mashuka kwa wagonjwa wodi zaidi ya 80, kandambili pamoja na kutoka msaada wa chakula, vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili.
---

No comments:
Post a Comment