WAMILIKI
wa nyumba aliyokuwa akiishi msanii wa Komedi, Hussein Mkieti ‘Sharo
Milionea’ wamesema watarudisha kiasi chote cha fedha ya kodi ya pango
kilichotolewa na nyota huyo.
Wakiongea
na Saluti5 jana, wamiliki hao wameahidi kukabidhi pesa zote za kodi ya
pango zilizokuwa zimelipwa na Sharo, siku vitakapokuwa vinatolewa
vyombo.
“Hatuwezi
kuzuia hela iliyotolewa na Sharo kama kodi ya pango kwa sababu kitendo
hicho ni sawa na dhuluma ambayo ni kosa kwa mujibu wa dini yetu ya
Kikristo,” walisema wamiliki hao.
Walisema
kuwa, watairudisha kodi hiyo kwasababu Sharo alihamia kwenye nyumba yao
takriban wiki moja tu kabla ya ajali iliyosababisha mauti kumfika.
SOURCE SALUTI5
No comments:
Post a Comment