Christiana Figueres.
 Mkuu wa Sekriterieti ya mabadiliko ya tabianchi ya Umoja wa Mataifa Christiana Figueres amewataka watu kutosubiri serikali zao kufanya maamuzi magumu ili kupunguza hali  ya ujoto duniani.
Kinyume na hilo, amewataka watafakari juu ya jukumu lao wenyewe katika kutatua tatizo hilo.
Christiana Figueres  amesema kuwa haoni kama jamii inaguswa na kuzisaidia serikali zao kuchukua maamuzi yenye nia ya dhati.