picha na maktaba
Vurugu
kubwa zinaendelea hivi sasa eneo la Dumila mkoani Morogoro, kufuatia
wananchi kufunga barabara ya Morogoro Dodoma, kwa kile wanachodai
kumtaka Mkuu wa Mkoa Joel Bendera kufika kuwatatulia tatizo lao la
kunyang'anywa maeneo yao ya wakulima na kuwapatia wafugaji.
Wananchi
hao wamegawanyika katika makundi kadhaa huku kila kundi likifunga
barabara ya kuingia na kutoka eneo hilo la Dumila, ambapo wamezuia
magari yote yanayopita eneo hilo kutoka moro na kotoka Dom, huku
wakichoma magari na kuvunja vioo vya magari hovyo, pamoja na kuchoma
moto nyumba za wageni na kuvunja vioo.
Tayari
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, ameomba udhuru kutoka katika Kikao cha wakuu
wa mikoa, kilichokuwa kikiendelea mkoani Dodoma, na hivi sasa yupo
njiani akielekea eneo hilo kwa nia ya kukutana na wananchi hao ili
kuwasikiliza na kutatua mgogoro huo.
No comments:
Post a Comment