Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, January 2, 2013

HUYU NDIO DADA YAKE MARIO BALOTELLI AMBAE YUKO MAPENZINI NA MCHEZAJI OBAFEMI MARTIN.



.
Kwa wiki kadhaa sasa hivi zimekuwepo taarifa kwamba mchezaji wa Manchester City Mario Balotelli amekasirishwa na kitendo cha mchezaji wa Nigeria Obafemi Martins kuingia kwenye mapenzi mazito na dada yake, yani dada wa Balotelli.
Obafemi ameamua kuzungumza kwa kusisitiza kwamba hizo ni habari tu kwamba Mario kakasirika lakini sio kweli, Balotelli anafurahi dada yake kuwa mapenzini na Obafemi.
Wapenzi hawa wamekua wakionekana sehemu mbalimbali za goodtimes na wameonekana wazi kabisa kuwa kwenye mapenzi mazito.
Obafemi amekaririwa na Daily Post akisisitiza kwamba “Mario ni mshkaji wangu, ananiheshimu na mimi namuheshimu… habari za yeye kukasirika ni watu tu wanatunga”
Balotelli
Obafemi amesema ni kweli yuko kwenye mapenzi mazito na Abigail lakini hawana mpango wa kuoana sasa hivi na wala hawajawahi kuliongelea hilo.
Kwenye interview na gazeti la The Sun April 2012 Abigail ambae ni dada wa Mario Balotelli alisisitiza kwamba hana mpango wa kuwa mapenzini na mchezaji yeyote wa mpira kwa sababu ni watu wanaozungukwa sana na wasichana, wasichana wanajipeleka wenyewe bila kuitwa, hata Balotelli hatomruhusu kuwa na mpenzi mwanasoka lakini naona mambo yamekua tofauti sasa hivi.

No comments:

Post a Comment