Sumalee akiwa Uingereza ambako alikwenda toka december 2012 akiwa na Barnaba.
Miezi 8 toka mama yake mzazi
afariki dunia, msanii wa bongofleva Sumalee amepata pigo jingine baada
ya baba yake mzazi kufariki january 31 2013.
Taarifa zilizoifikia dj-sek.blogspot.com ni kwamba baba yake alifariki jana jioni wakati bado Sumalee yuko Uingereza kwa shughuli za kimuziki.
Namkariri akisema “mama yangu amekufa kwenye mikono yangu, yuko kwenye mapaja yangu na mikononi nilikua namsomea dua tu”
Kulikua kuna taarifa kwamba
Sumalee kapata matatizo ya hati yake ya kusafiria huko Uingereza hivyo
itakua ngumu kuja Tanzania msibani lakini taarifa nilizonazo kutoka kwa
mtu wa karibu ni kwamba hajapata tatizo lolote kama wengi wanavyodhani,
kilichotokea ni kwamba alitaka kuongeza miezi sita ya kuendelea kukaa
Uingereza hivyo ikabidi Passport aiache ubalozini ambapo ghafla ndio
akapata msiba hivyo itabidi asafiri kwa kutumia documents.
Mtu huyu wa karibu wa Sumalee
ameiambia dj-sek.blogspot.com kwamba baba mzazi wa Sumalee anazikwa leo
february 1 2013 na Sumalee wamejaribu kuwasiliana nae hapatikani kwenye
simu hivyo hakuna uhakika kama yuko kwenye ndege kuja Tanzania ama la.
dj-sek.blogspot.com inatoa pole kwa Sumalee, familia na ndugu kwa msiba huu.
No comments:
Post a Comment