Pichani katikati ni Mwenyekiti wa kamati ya Tuzo za wanawake wenye Mafanikio Tanzania bi. Sadaka Gandi akifafanua jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na mchakato mzima wa tuzo hizo, kulia Raisi wa tuzo hizo bi. Irene Kiwia na kushoto ni bi. Esther Shayo mratibu.
Pichani kulia ni Raisi wa tuzo hizo Irene Kiwia akielezea jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),kuhusiana na tuzo hizo za Wanawake
wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013, zilizopangwa kufanyika katika
siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu.
Taasisi
ya Tanzania Women of Achievement (TWAA) leo imezindua Tuzo za Wanawake
wenye Mafanikio Tanzania msimu wa 2013 zilizopangwa kufanyika katika
siku ya wanawake duniani tarehe 8 Mwezi Machi mwaka huu. Tuzo
hizi ambazo hufanyika kila baada ya miaka miwili zilizinduliwa mwaka
2009 kwa heshima ya wanawake katika sekta mbalimbali nchini kote ambao
kupitia kazi zao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana kuleta maendeleo ya
jamii zao kwa njia moja au nyingine.
"TWAA
inataka kutambua wanawake, waishio Tanzania ambao kupitia kazi zao
wameweza kupata mafanikio makubwa si tu kibinafsi bali wametumia nafasi
zao kuleta maendeleo na mabadiliko ya kimsingi kwenye jamii
zinazowazunguka." Alisema Mkurugenzi mkuu wa TWA Bi. Irene Kiwia. "Tuzo
hizi mbazo sasa ziko katika msimu wake wa 3 zinatoa fursa nzuri ya
kutambua na kupongeza wanawake ambao wamechangia sana kwenye kubadilisha
na kuboresha sura ya Tanzania. Kwa wanawake wengi hii itakuwa mara ya
kwanza mafanikio na michango yao imetunukiwa na hili ni jambo la
kufariji na kuridhisha sana.”
Vipengele
vya tuzo za mwaka huu ni Sanaa na Utamaduni, Biashara na Ujasiriamali,
Habari na Mawasiliano, Michezo, Professional (Kazi), Elimu, Afya, Ustawi
wa Jamii, Sayansi naTeknolojia, Sekta ya Umma, Kilimo na Mshiriko
Mdogo.
Bi
SadakaGandi, mwenyekiti wa kamati ya TWAA alitoa wito kuwa "tunawasihi
mashirika, vyama, wanawake na wanaume kote Tanzania kuteuawa na wake
wenye mafanikio katika makundi haya na kuonyesha mchango wao katika
uwezeshaji wa wanawake. Kuna maelfu ya wanawake wastahili watuzo hizi
huko nje ambao ni mawakala wamabadiliko katika jamii zao.
Tunataka
kuimba mapambio ya mashujaa hawa na kuhamasisha mamilioni ya wanawake
wengine wa Tanzania kuiga mifano na kupata msukumo wa kuleta mabadiliko.
Kamati ilipokea fomu nyingi sana za washiriki miaka ya nyuma na hivyo
basi tunategemea ushiriki mzuri zaidi mwaka huu. "
Kamati
ya TWAA inawajumuisha Bi Mary Rusimbi – Mwanaharakati na Mwanzilishi wa
Programu yaMtandao wa Jinsia Tanzania, Jaji Joaquine De Mello –
Kamishna waTume ya Hakiza Binadamu naUtawala Bora, Dk Marcelina
Chijoriga-Mkurugenzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bi.Ludovicka
Tarimo–Mtaalamu wa Jinsia kutoka USAID, Bwana. Innocent Mungy-Mkurugenzi
wa Mawasiliano kutoka Mamlakaya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania
(TCRA), Sadaka Gandi – Mwanasaikolojia na mfanyakazi za Jamii, Irene
Kiwia – Mwanzilishi na Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya mahusiano ya jamii Frontline Porter Novelli.
Mtendaji wa kampuni ya mahusiano ya jamii Frontline Porter Novelli.
Huko
nyuma tuzo hizi zilidhaminiwana Baileys, Delloite, NBC, Home Shopping
Center, TCRA, Songas, WatuwaMarekani, DTP, UN DPG Gender Group, UNFPA,
UNESCO, TBL, Multichoice, African Life Assurance, Barrick, Twiga Cement,
Vodacom, Farm Equip, RBP, Clouds FM na Frontline Porter Novelli.
No comments:
Post a Comment