Omba omba tapeli anayejifanya hana mikono akikamatwa na wananchi baada ya kukimbia
Hapa akibanwa kuonyesha mikono yake yote miwili
Wananchi eneo la Miyomboni wakiwa wamembana omba omba huyu tapeli kuonyesha mikono yake yote
'' Huwa unasema wewe ni mlemavu huna mkono mmoja hii nini ....nyosha juu watu waone utapeli wako"
Hapa kipigo kilipoanza kwa mzee huyo tapeli anayejifanya hana mkono mmoja na mguu
Hapa ni kipigo kikiendelea
Hapa baada ya kupata upenyo akivaa nguo zake
Hapa akiwa ameachiwa na kuanza kutimua mbio
Baada ya kuchezea kichapo tapeli huyo sasa anajaribu kuficha aibu
OMBA OMBA ALIYEIGIZA MLEMAVU WA MIGUU NA MIKONO ATIMUA MBIO
Huyu ni omba
omba anayeigiza kutokuwa na mkono mmoja na mguu akiwa ameka eneo la M.R
akisubiri kuomba chochote kutoka kwa wapita njia leo
Hapa akisubiri msaada kutoka kwa wasamaria wema leo
Hapa akitimua mbio kukwepa kamera ya mtandao huu leo
AMA Kweli
mwisho wa utapeli ni aibu kubwa na wahenga walinena kuwa
ukistaajabu ya mussa utayaona ya filauni leo kwa wakazi wa Miyomboni
mjini Iringa wamepata kushuhudia kituko cha mwaka baada ya watu
waliochoka kuvumilia vitendo vya kitapeli vinavyofanywa mzee mmoha
ambae amekuwa akiigiza ni mlemavu asiye na mguu mmoja na mkono mmoja.
Tapeli
huyo mbali ya kuumbuliwa kwa kutakiwa kuonyesha miguu yake yote
pamoja na mikono yake yote bado amepata kuchezea kichapo kiasi
cha kunusurika kuuwawa na wananchi hao wenye hasira kali.
ndio ulipata kufichua siri hiyo ya omba omba huyo kuwa si omba omba kutokana na kumnasa akijiweka mfano wa mlemavu .
Kutokana na
kufichuliwa kwa siri hiyo ya kujiigiza kuwa ni omba omba mlemavu
wananchi wamekuwa wakimtimua kila kona anayokaa tapeli huyo na
kumtimua mbio kabla ya leo wananchi hao kuamua kumkimbiza kutoka eneo
la Hazina Ndogo hadi miyomboni na kuanza kumpa kichapo hadi
alipoamua kuonyesha viungo vyote kuwa si mlemavu
Tapeli huyo
mbali ya kujifanya ni mlemavu wa viungo wakati mwingine huwa
anajifanya ni mtu asiyeongea (bubu) asiye na viungo kama mikono na
miguu ila wakati mwingine akijifanya ni hana mguu mmoja na kuwaomba
watu fedha za matibabu .
Hata hivyo
baada ya mmoja kati ya wananchi kufika eneo hilo alionyesha kufichua
mbinu hiyo chafu ya mzee huyo kujifanya ni mlemavu wakati asubuhi
alikutana maeneo akiwa mzima wa afya njema na katika kumhoji zaidi ndipo
kamera ya mtandao huu ilipoamua kufanya kazi yake ya kunasa kituko
hicho na ndipo mzee huyo alipoanza kuongea kwa sauti vizuri tofauti na
alivyokuwa akijifanya kuwa hawezi kuongea kabisa (bubu)
Wakati
mabishano yakiendelea eneo hilo ghafla mzee huyo alisimama kwa miguu
yake yote miwili pamoja na awali kujifanya ni mlemavu asiye na mguu
mmoja ila baada ya watu kutaka apigwe picha ndipo mzee huyo alipoanza
kutimua mbio huku ulemavu aliokuwa nao akiusahau hapo kutokana na
kichapo alichokipata na kuumizwa vibaya usoni .
Hata hivyo
inasemekana mzee huyo amekuwa akiadhibuwa katika maeneo mbali mbali
kutokana na mbinu yake ya kufuru anayoifanya kuwa ni mlemavu wakati
si mlemavu na kuwa ni heri kuomba kama mtu mwenye matatizo ya kiuchumi
kuliko kuwaigiza walemavu na kuwa iwapo atarudia na kukutwa
akifanya hivyo watamvunja kweli mkono ili kuwa mlemavu walisema
wananchi hao ambao hata hivyo mtandao huu uliwaomba kufanya hivyo .
Aidha
anadaiwa chanzo cha kichapo cha leo kwa mzee huyo tapeli ni mmoja
kati ya mpenzi wake ambae alikuwa amemsusa na kuhamia kwa mpenzi
mwingine kuueleza umma kuwa huyo ni tapeli na yeye ni mpenzi wake
ambae anamtambua kuwa na miguu yote,mikono na si bubu kama
anavyoigiza jambo lililopelekea wananchi kufanya udadisi .
Kabla
kufukuzwa na kuchezea kichapo tapeli huyo alifukuzwa eneo ambalo
alikuwa amekaa barabara eneo la Santona na kutoka kuondoka haraka na
mmoja kati ya vijana wanaofanya kazi ya kusafisha na kushona viatu na
kupuuza na ndipo mtiti ulipoanza.
Baadhi ya
wananchi wameuomba uongozi wa Manispaa ya Iringa kuwabana omba omba hao
ambao wamekuwa wakidanganya watu kuwa wao ni walemavu kumbe ni wazima na
kutaka kuwepo kwa utaratibu maalum wa watu kuomba misaada. CHANZO
FRANCIS GODWIN
No comments:
Post a Comment