Lori la
mafuta likiwa limelidondokea gari ndogo baada ya kutoka ajali katika
eneo la Chang'aombe jinini Dar es salaam ikihusisha na daladala ya abiria.
Ajali mbaya inayohusisha Lori la Mafuta, Daladala pamoja na Gari aina
ya Prado imetokea muda mfupi uliopita maeneo ya Chang'ombe Machinjioni
kwenye mataa Jijini Dar es Salaam baada ya dereva wa dalalala ambayo
haikuwa na abiria
kuingia vibaya katika makutano ya barabara na kusababisha dereva wa
lori kugonga daladala na kuangukia Prado hii wakati akijaribu kukwepa
kusababisha madhara.
Hakuna mtu yoyote aliyepoteza maisha
katika tukio ili isipokuwa majeraha ya kawaida yamewapata madereva
husika, Wananchi wameonekana eneo la tukio wakichota mafuta ya mawese
yaliyomwagika kutoka kwenye lori lililopata ajali na mpaka sasa hatua
zote za tahadhari zimeshachukuliwa
No comments:
Post a Comment