JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani ya Simu “MKUUPOLISI” & nbsp; Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734 Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556 S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja: DAR ES SALAAM.
26 MAY 2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Kwa
mafanikio makubwa, Jeshi la Polisi nchini limeendelea kuwakamata
wachochezi wanaotumia simu za mkononi (sms) ili kuchochea vurugu na fujo
hapa nchini ambapo huko mkoani Lindi amekamatwa mtu mwingine mmoja kwa
kufanya uhalifu huo.
Aidha,
katika hatua nyingine, mtu aliyekamatwa jijini Dar es Salaam kwa tuhuma
za kutuma meseji za uchochezi na kuhamasisha vurugu, Jeshi la Polisi
limekamilisha upelelezi na ukusanyaji wa ushahidi na kesho atafikishwa
makahamani.
Jeshi
la Polisi linaendelea kukamilisha ukusanyaji wa ushahidi wa watu
wanaofadhili, wanaosaidia na wanaoshawishi vitendo hivyo kutekelezwa ili
na wao wafikishwe mahakamani mapema.
Katika
kuhakikisha kwamba vitendo hivyo vinakomeshwa na kudhibitiwa hapa
nchini, Jeshi la Polisi limeunda kikosi maalum toka makao makuu kwenda
kusaidiana na makamanda wa mikoa ili kwa kusaidiana na wananchi kuweza
kuharakisha ukamataji na watu wote wanaojihusisha na uchochezi wa vurugu
na fujo kwa njia ya sms na kwa njia nyingine yeyote ile popote walipo
ili waweze kufikishwa mahakamani haraka.
Jeshi
la Polisi linawashukuru wananchi kwa ushirikiano wao mkubwa wa kutoa
taarifa zinazofanikisha oparesheni hii, tunaomba waendelee kutuunga
mkono kwa kutupatia taarifa zaidi na hata za watu wanaofadhili kwa njia
ya pesa ama ushauri.
Jeshi
la Polisi linatoa onyo kali kwa mtu yeyote ama kikundi cha watu
wanaojihusisha na vitendo hivyo vya uchochezi kuacha mara moja. Aidha,
litamkamata mtu yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo vya uchochezi
bila woga ama upendeleo pasipo kujali cheo, wadhifa, rangi ama umaarufu
wa mtu huyo.
Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (TZ)
TAARIFA YA JANA YA KIPOLISI NI HII HAPA ....
No comments:
Post a Comment