Dar es Salaam. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato
cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za
viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini.
Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema
matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha
ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo
hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la
nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na
huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao
82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali
sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012
watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126
sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.
Msemaji wa Necta, John Nchimbi alisema upangaji wa
matokeo hayo ulikuwa bado unaendelea. “Ninachojua kwa sasa ni kuwa
mchakato unaendelea na matokeo yatatangazwa mapema tu ili watoto waweze
kujiunga na shule mapema,” alisema Nchimbi.
Pia alisema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha sita umekamilika.
Matokeo ya awali
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu
na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya
watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana,
waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847
sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa
na asilimia 28.1.
Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na
asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo
mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100
ambayo ni asilimia 43.
Hata hivyo, habari kutoka Necta zinasema kuwa
licha ya kuwezesha kuongezeka kwa waliofaulu, matumizi ya kanuni mpya ya
kukokotoa matokeo hayo yalisababisha zaidi ya wanafunzi 2,500 kushuka
ufaulu ikilinganishwa na awali.
Maofisa mbalimbali wa Necta pamoja na wale wa
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake, walikutana
mwishoni mwa wiki iliyopita kukubaliana masuala mbalimbali juu ya
matokeo hayo pamoja na suala la matokeo ya wanafunzi hao 2,500 kabla ya
kutangazwa wiki hii.
“Baada ya wajumbe kujadili suala lile, busara
ilibidi itumike kwa hiyo hakuna mwanafunzi ambaye alama yake itashuka,
kwa kawaida isingewezekana mtoto ambaye matokeo yalitoka akiwa amefaulu
leo umwambie ameshuka,” kilieleza chanzo chetu.
source Mwananchi
source Mwananchi
No comments:
Post a Comment