Gareth Bale akikabidhiwa jezi namba 11 na Rais wa Real Madrid Florentino Perez kwenye Uwanja wa Bernabeu muda mfupi uliopita.
-AJIUNGA MADRID KWA BILIONI 216-KULIPWA MILIONI 644.6 KWA WIKI
- USAJILI WAKE WAZIDI WA RONALDO KWA BILIONI 15.3
Gareth Bale ametua rasmi katika klabu ya Real Madrid kwa uhamisho uliovunja rekodi ya dunia. Bale amejiunga na Madrid kwa Pauni milioni 86 sawa na shilingi bilioni 216.7 za Tanzania. Ametua jana usiku nchini Hispania kwa vipimo vya leo asubuhi kabla hajatambulishwa kwa mashabiki. Mchezaji huo amempiku mshambuliaji wa timu hiyo kutoka nchini Ureno, Cristiano Ronaldo aliyesajiliwa kwa Pauni milioni 80 sawa na shilingi bilioni 201.4 za Tanzania mwaka 2009 akitokea klabu ya Manchester United.
Bale amesajiliwa kwa mkataba wa miaka sita na atakuwa akilipwa pauni 256,000 sawa na shilingi milioni 644.6 za Tanzania kwa wiki.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Wales ameishukuru timu yake ya zamani ya Tottenham Hotspur alipodumu kwa miaka sita. Mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy na Meneja wa timu hiyo Andre Villas-Boas wamemtakia kila la kheri staa huyo.
Bale atalipwa kama ifuatavyo:
33,520,281,600 Kwa mwaka
91,835,801 kwa siku
3,827,436 kwa saa
63,840 kwa dakika
1064 kwa sekunde
No comments:
Post a Comment