NGULI wa muziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ ameanza
kuugua tena ambapo tangu Sikukuu ya Iddi hadi sasa yupo hoi kitandani.
Akizungumza kwa huzuni na mwandishi wetu, Banza alisema alipomaliza shoo
ya Sikukuu ya Iddi na Bendi ya Extra Bongo, alianza kuugua, akaenda
Hospitali ya Yemen iliyopo Sinza, Dar ikagundulika ana malaria kali
ambapo alipewa dozi ya siku saba.
“Nilipewa dawa za malaria nikameza nikaambiwa baada ya siku saba
nitajisikia vizuri lakini mpaka sasa sioni mabadiliko yoyote, bado mwili
unaniuma sana, nashinda kitandani kila siku hivyo muziki basi kwa
sasa,” alisema Banza na kuongeza:
“Najua mashabiki wangu watanimisi lakini kwa sasa muziki nimepumzika, naomba mashabiki waniombee.”
No comments:
Post a Comment