Baadhi ya
vyombo vya habari nchini jana na leo vimekuwa vikiripoti juu ya tukio
la kuuwawa na tembo kwa mgeni kutoka Marekani anayefahamika kama Thomas
Vardon Macfee (58) tarehe 31.08.2013 katika Hifadhi ya Taifa Tarangire.
Shirika la Hifadhi za Taifa linapenda kuweka usahihi wa taarifa zilizoripotiwa kama ifutavyo:-
Tukio la mgeni husika lilitokea nje ya Hifadhi ya Tarangire katika kijiji cha Kakoi kambi ya Tarangire River Camp, wakiwa wanafanya utalii wa kutembea kwa miguu "Walking Safari". Baada ya kuvamiwa nakuumizwa, mgeni huyu alifikishwa katika zahanati ya Hifadhi ya Tarangire na watumishi wa kambi aliyofikia iliyo nje ya hifadhi kwa ajili ya matibabu ya huduma ya kwanza na alipofikishwa, alifariki dunia.
Hivyo basi, Shirika linapenda kusahihisha kuwa tukio lililopelekea kifo cha mgeni lilitokea nje ya Hifadhi ya Tarangire na si ndani kama ilivyoripotiwa.
IMETOLEWA NA IDARA YA UHUSIANO
HIFADHI ZA TAIFA
S.L.P 3134
ARUSHA
05/09/2013
HIFADHI ZA TAIFA
S.L.P 3134
ARUSHA
05/09/2013
No comments:
Post a Comment