NYAMLANI (MWENYE TAI) |
Wagombea wawili, Athumani Nyamlani na Jamal Malinzi wamepitishwa kuwania nafasi ya Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
MALINZI |
Malinzi na Nyamlani ambaye anashikilia nafasi ya Makamu wa Kwanza wa
Rais wa TFF, wamepitishwa baada ya usaili uliofanyika jijini Dar es
Salaam.
Upinzani kati ya Nyamlani na Malinzi umekuwa mkali sana tokea walipotangaza tu kugombea.
Katika nafasi hiyo kulikuwa na wagombea wanne na wawili kati yao hawakupita ambao ni Omary Mussa na Richard Lukambula.
Kwa
upande wa umakamu wa urais, Wallace Karia na Iman Madega, mwenyekiti wa
zamani wa Yanga, ndiyo waliopitishwa kuwania nafasi hiyo.
Wakati huohuo, usaili huo pia umemng’oa Shaffi Dauda aliyekuwa nawania ujumbe.
No comments:
Post a Comment