KWELI
dunia inakwenda ukingoni, mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu,
amefanya kitendo cha kinyama baada ya kujifungua msalani na kukiua
kichanga chake.
Tukio
hilo limetokea hivi karibuni maeneo ya Mazizini, Ukonga Wilaya ya Ilala
jijini Dar es Salaam baada ya mwanamke huyo ambaye jina lake
halikupatikana kukitumbukiza kichanga hicho chooni.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, mwanamke huyo ni mkazi wa Ukonga Moshi Bar
alidaiwa kunywa dawa kwa ajili ya kuutoa ujauzito aliokuwa nao wa miezi
minane na baada ya kuona hali imebadilika alitoka nyumbani kwake Moshi
Bar na kukimbilia Ukonga Mazizini kwa ajili ya kutaka msaada kwa mama
yake mdogo.
Baada
ya kufika kwa mama yake mdogo aliomba maji kwa ajili ya kwenda chooni,
hata hivyo alizunguka nyuma ya choo kwa ajili ya kujipa msaada wa siri
lakini hali ilivyokuwa mbaya zaidi, aliamua kuingia ndani ya choo hicho
na kujifungua kichanga hicho na kukidumbukiza ndani ya shimo la choo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa walimuona mwanamke huyo
akibebwa kwenda ndani kwa mama yake mdogo ili aweze kupatiwa msaada
zaidi lakini hali ilizidi kuwa mbaya kwa kuanza kuvimba mwili kutokana
na kutokwa na damu nyingi.
Waandishi
wetu walifanikiwa kuzungumza na mama mdogo wa mwanamke huyo ambaye
alijitambulisha kwa jina la mama Athony alikiri binti huyo kukumbwa na
mkasa huo wakati yeye akiwa kwenye shughuli zake.
“Kweli
nafahamu, alikuwa ni mjamzito na alifika nyumbani kwangu saa tano
asubuhi, alichokifanya hapa si kitu cha bahati mbaya ni makusudi,”
alisema mama huyo.
Mama
Antony alisema kuwa wakati anarudi nyumbani aliukuta umati wa watu na
alipoingia ndani ndipo alipopewa habari za tukio hilo.
Alipotakiwa
kutaja jina la binti huyo, mama huyo alianza kuangua kilio na
kuwafanya waandishi wetu washindwe kuendelea na mahojiano naye.
Mwakilishi
wa mjumbe na shina namba 34 Ukonga Mazizini, Bi Mtende alisema kuwa
tukio hilo limewashangaza kutokana na mwanamke huyo kwenda kutupa
kichanga chooni kwa makusudi.
Bi Mtende alisema kwanza mwanamke huyo siyo mkazi wa maeneo hayo, hivyo hakuna aliyeweza kumjua kwa jina.
Kikosi cha zimamoto na uokoaji kilifika katika eneo hilo majira ya saa saba mchana kwa ajili ya kutimiza wajibu wao
Kikosi
hicho kikiwa kimesheheni zana za uokoaji kilikuta kichanga hicho
kikielea chooni na kwa kutumia mbinu zao za uokoaji na walifanikiwa
kukitoa kichanga hicho kikiwa kikiwa maiti.
Kamanda
wa polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ACP Marietha Minangi alikiri
kutokea kwa tukio hilo ambalo yeye aliliita ni la kikatili na mwanamke
huyo amepelekwa katika Hospitali ya Amana kwa matibabu na mwili wa
kichanga hicho kimepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa
uchunguzi zaidi.
Waandishi wetu walifika katika Hospitali ya Amana kwa ajili ya kupata mahojiano na mama huyo Jumanne iliyopita, hata hivyo
No comments:
Post a Comment