Citizen
TV Kenya wanaripoti kwamba huko Mombasa wamekamatwa watu 26 wenye
ulemavu ambao walichukuliwa kutoka Tanzania na Mwanamke Mtanzania ili
kwenda kufanya biashara ya kuomba pesa na baadae jioni Mwanamke huyo
anapitia mahesabu huku akiwa amewaweka walemavu hawa kuishi kwenye
nyumba moja huko Mwembe tayari.
Mwanamke
huyu nadaiwa kuwa na mtindo wa kuagiza Walemavu kuchukuliwa Tanzania na
kuingizwa Kenya kupitia Taveta na Lungalunga ambapo anawatumia
kibiashara yeye na washirika wake ambapo mpaka sasa washukiwa saba
wametiwa mbaroni kutokana na hii ishu.
Taarifa
inasema ombaomba hawa ambao wanatoka Shinyanga, Mwanza, Musoma na
Bukoba wakiwa mitaani kuomba, wakipata shilingi mia tano ya Kenya tajiri
anachukua shilingi 300 na anamuachia shilingi 200.
Mmoja
wa Walemavu hao anasema ‘kabla ya kuletwa Kenya tunapewa ahadi nzuri za
kuvutia kwenda, mimi niliahidiwa kupewa Baiskeli lakini kinachotokea
sasa hivi ni kwamba nikipata hiyo pesa ya kuombaomba, Mwanamke huyu ndio
anapanga bajeti zake wala hamna anachofanya’
Angalia video:
No comments:
Post a Comment