Cobb amekuwa mzungu wa kwanza aliyejitokeza hadharani kutaka taifa lenye mlengo wa kibaguzi dhidi ya weusi .
Mwaka 1960 mtunga filamu wa Uingereza, John
Carpenter alitoa sinema iliyoitwa Kijiji cha Waliolaanika, lakini mwaka
1995 Mmarekani John Wyndham naye alitunga sinema yenye jina kama hilo
iliyoandaliwa California Kaskazini nchini Marekani.
Hata hivyo, Mmarekani Craig Paul Cobb ametumia
jina hilo la ‘Kijiji cha Waliolaanika’ kutaka kuanzisha eneo lenye
ubaguzi ndani ya Marekani, akiita ‘taifa jipya’. Kisa kuwaita kijiji
kilicholaanika ni kwa sababu ya mwanamke wa kizungu kuolewa na mweusi.
Cobb kama anavyotambulika na wengi alizaliwa
Oktoba 9, 1951, kwa sasa ana umri wa miaka 62, akiwa na uraia wa nchi
mbili, Marekani na Canada, imani yake ya kidini ni uanaharakati, sasa
amepanga kuugeuza mji mdogo wa Leith, Dakota Kaskazini kuwa ‘pepo ya
wazungu wenye imani kali, wasiopenda kuchanganyika na watu weusi.
Mji wa Leith una mwanaume mmoja mweusi ambaye
ameoa mzungu, Bobby Harper na mkewe Sherill wameishi katika mji huo kwa
miongo miwili. Na wameweka bango kwenye mlango wa nyumba yao likisema,
“Mtafanya nini kwa mwanamke aliyeolewa na Mnegro?’
Ubabe wa Kynan Dutton
Hata hivyo, Dutton aliweka bango jirani na
wanandoa hao likiwa na maandishi yaliyosomeka; “Nataka umuache mume wako
na kuungana na chama cha Cobb. Fanya hivyo sasa.’
Bobby amesema ameamua kununua bunduki pia amemnunulia mkewe bunduki, wakijiweka tayari na uvamizi wa wafuasi wa Cobb.
Cobb aliyewahi kuishi Vancouver nchini Canada,
amehamia katika mji mdogo wa Leith alikonunua magofu 12, ametangaza
kuufanya mji huo kuwa ‘taifa jipya la wazungu’ na ameweka bango kubwa
kwenye mpaka wa eneo lake na wenyeji lenye maneno ya kuwatuhumu wenyeji
kuwa ‘Kijiji cha Waliolaanika.’
Historia ya Cobb inaonyesha ni mbaguzi, Juni 2010
alikamatwa mjini Vancouver kwa kuandika habari za kuchochea ubaguzi
kwenye tovuti yake. Alitoka kwa dhamana na aliitoroka nchi hiyo kabla ya
kufikishwa mahakamani Desemba 2010 kwa tuhuma za uchochezi.
Kiongozi wa Kaunti ya Grant, Steve Bay katika
taarifa amesema wamepata taarifa ya mipango ya Cobb ya kutaka
kujimilikisha Mji wa Leith. Amesema amekuwa akipigiwa simu na wenyeji wa
Leith wakielezea hofu iliyotanda kwamba Cobb anataka kujimilikisha mji
huo na kuanzisha sheria za kutawala eneo hilo kwa misingi ya ubaguzi.CHANZO MWANAINCHI
No comments:
Post a Comment