Pages

Saturday, November 9, 2013

DUNIANI MAMBO NA VIJIMAMBO::Ataka kuanzisha ‘taifa la wazungu’ wenye imani kali ya ubaguzi wa rangi


Craig Paul Cobb akizunguka kwenye eneo la makazi yake katika mji wa Leith . Picha na Maktaba 

Cobb amekuwa mzungu wa kwanza aliyejitokeza hadharani kutaka taifa lenye mlengo wa kibaguzi dhidi ya weusi .
Mwaka 1960 mtunga filamu wa Uingereza, John Carpenter alitoa sinema iliyoitwa Kijiji cha Waliolaanika, lakini mwaka 1995 Mmarekani John Wyndham naye alitunga sinema yenye jina kama hilo iliyoandaliwa California Kaskazini nchini Marekani.
Hata hivyo, Mmarekani Craig Paul Cobb ametumia jina hilo la ‘Kijiji cha Waliolaanika’ kutaka kuanzisha eneo lenye ubaguzi ndani ya Marekani, akiita ‘taifa jipya’. Kisa kuwaita kijiji kilicholaanika ni kwa sababu ya mwanamke wa kizungu kuolewa na mweusi.
Cobb kama anavyotambulika na wengi alizaliwa Oktoba 9, 1951, kwa sasa ana umri wa miaka 62, akiwa na uraia wa nchi mbili, Marekani na Canada, imani yake ya kidini ni uanaharakati, sasa amepanga kuugeuza mji mdogo wa Leith, Dakota Kaskazini kuwa ‘pepo ya wazungu wenye imani kali, wasiopenda kuchanganyika na watu weusi.
Mji wa Leith una mwanaume mmoja mweusi ambaye ameoa mzungu, Bobby Harper na mkewe Sherill wameishi katika mji huo kwa miongo miwili. Na wameweka bango kwenye mlango wa nyumba yao likisema, “Mtafanya nini kwa mwanamke aliyeolewa na Mnegro?’
Ubabe wa Kynan Dutton
Hata hivyo, Dutton aliweka bango jirani na wanandoa hao likiwa na maandishi yaliyosomeka; “Nataka umuache mume wako na kuungana na chama cha Cobb. Fanya hivyo sasa.’
Bobby amesema ameamua kununua bunduki pia amemnunulia mkewe bunduki, wakijiweka tayari na uvamizi wa wafuasi wa Cobb.
Cobb aliyewahi kuishi Vancouver nchini Canada, amehamia katika mji mdogo wa Leith alikonunua magofu 12, ametangaza kuufanya mji huo kuwa ‘taifa jipya la wazungu’ na ameweka bango kubwa kwenye mpaka wa eneo lake na wenyeji lenye maneno ya kuwatuhumu wenyeji kuwa ‘Kijiji cha Waliolaanika.’
Historia ya Cobb inaonyesha ni mbaguzi, Juni 2010 alikamatwa mjini Vancouver kwa kuandika habari za kuchochea ubaguzi kwenye tovuti yake. Alitoka kwa dhamana na aliitoroka nchi hiyo kabla ya kufikishwa mahakamani Desemba 2010 kwa tuhuma za uchochezi.
Kiongozi wa Kaunti ya Grant, Steve Bay katika taarifa amesema wamepata taarifa ya mipango ya Cobb ya kutaka kujimilikisha Mji wa Leith. Amesema amekuwa akipigiwa simu na wenyeji wa Leith wakielezea hofu iliyotanda kwamba Cobb anataka kujimilikisha mji huo na kuanzisha sheria za kutawala eneo hilo kwa misingi ya ubaguzi.CHANZO MWANAINCHI

No comments:

Post a Comment