Mabadiliko hayo yanatarajiwa kufanyika mara baada
ya wakuu mbalimbali wa Idara kumaliza muda wao ifikapo Desemba 31 mwaka
huu na hakuna mpango wa kuwaongezea mkataba baadhi ya wakuu wa idara
hao.
Habari za uhakika kutoka kwa mmoja wa viongzi wa
juu wa TFF zilisema kuwa shirikisho hilo linatarajia kutangaza nafasi za
kazi kwa upande wa wakuu wa Idara ifikapo Novemba 15 na mpaka sasa,
kitengo cha habari chini ya Ofrisa Habari, Boniface Wambura pekee ndicho
hakitaathirika na mabadiliko hayo.
Hatua ya kumbakiza Wambura inatokana na ufanisi
katika kazi yake na kuvutiwa na Kamati ya Utendaji na kufikia hatua ya
kumteua kuwa Kaimu Katibu Mkuu baada ya kupewa likizo yenye malipo kwa
aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo, Angetile Osiah.
Taarifa hizo zimesema kuwa Wambura anapigiwa chapuo kubwa kushika wadhifa huo kutokana na utendaji wake bora wa kazi.
“Tumeamua kufanya kazi ya kuleta maendeleo katika
soka la Tanzania, hivyo chukulieni mabadiliko haya ni ya kawaida na hasa
kwa uongozi ambao unataka kuweka historia ya maendeleo ya soka nchini.
“Mabadiliko hayana muda maalum, hakuna cha
kusubiri kwani mtu anapimwa kutokana na ufanisi wake na wala si
vinginevyo, kuna watu wamesema mamuzi ya kumsimamisha Katibu Mkuu ni ya
kisasi, siyo kweli kwani ni maamuzi ya pamoja,” alisema mmoja wa
viongozi wa TFF.
Alisema kuwa kampuni ya KPMG inatarajiwa kupewa
kazi ya kuwatafuta wafanyakazi wapya (wakuu wa idara) wa shirikisho hilo
na kuwataka wadau wa michezo kukaa ‘mkao wa kula’ ili kutuma maombi
yao.
Nafasi ambazo zinatarajiwa kutangazwa ni
Mkurugenzi wa Idara ya Fedha ambayo ipo chini ya Kaimu Mkurugenzi,
Yonaza Seleki, Mkurugenzi wa Utawala na Wanachama (tupu), Mkurugenzi wa
Mashindano (Saad Kawemba), Mkurugenzi wa Masoko na Matukio (James Kabwe)
na Mkurugenzi wa Ufundi iliyo chini ya kocha maarufu Sunday Kayuni.CHANZO MWANANCHI
No comments:
Post a Comment