Kampuni
ya LG ya Korea Kusini imetoa simu mpya LG G Flex zilizotengenezwa kwa
material yanayoziwezesha simu hizo kurudi katika hali yake ya upya, hata
baada ya kupata mikwaruzo ya kawaida ambayo hufanya simu ionekane
kuchakaa. Simu hizo zina uwezo wa kujirudisha katika hali ya kawaida
(self-healing) mara baada ya kupata mikwaruzo ya kitu chenye ncha kama
funguo, kisu nk, na baada ya muda alama zote za mikwaruzo zinapotea na
kurudi ilivyokuwa.
Pia
display ya simu hizo za LG G Flex imetengenezwa kwa plastic badala ya
kioo kama zilivyo simu zingine, na pia muundo wake wa kujikunja (curve)
unairuhusu simu kunyooka pindi inapokandamizwa kwa nguvu na kurudi
katika hali yake bila kuvunjika.
Kwa
simu hizi za G Flex, mtumiaji hatapata yale maumivu ambayo huwakuta
watumiaji wengi ya kuvunjika kwa kioo, au simu kupata mikwaruzo mingi
inayosababisha kuifanya ichakae haraka.
GG
Flex ambazo kwa sasa zinapatikana Korea peke yake zitazinduliwa kwa
soko la kimataifa Jumanne ijayo (December 3) huko Hong Kong. Bei ya
simu hizo kwa Korea ni 999,990KRW sawa na Tsh milioni moja na nusu.
Tazama video kujionea majaribio ya G Flex
No comments:
Post a Comment