Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, November 9, 2013

JE MWISHO WA UTEJA WA MIAKA 10 WA ARSENAL KWA MAN UNITED UMEWADIA?


article-2492557-1949D60F00000578-262_634x452_377d1.jpg
ILIKUWA Novemba 28, mwaka 2011, Arsenal ilipoondoka imetota vibaya Uwanja wa Old Trafford ikitandikwa mabao 8-2, siku ambayo Wayne Rooney alifunga Hat-trick na Ashley Young akafunga mawili. Danny Welbeck pia alifunga.
Kwa kiasi kikubwa Arsenal imekuwa ikinyanyaswa na Mashetani hao Wekundu, wakiwa wameweza kushinda mechi moja tu ndani ya misimu 10 na wao wakifungwa mechi 11.
Man United 2-1 Arsenal, Ligi Kuu Novemba 3, 2012
Van Persie alihitaji dakika tu kuwakumbusha mashabiki wa Arsenal kipi watakosa kwa kuuzwa kwake kwa Pauni Milioni 24 kwenda Old Trafford, akifunga bao la kwanza kwa guu la kulia. Patrice Evra akaifungia la pili United baada ya mapumziko na Santi Cazorla akaipatia bao la kufutia machozi Arsenal. Kipigo hicho kiliwaacha Arsenal na pointi 15 baada ya mechi 10, mwanzo mbaya zaidi katika historia yao kwenye Ligi Kuu ya England chini ya Wenger.
Man United 8-2 Arsenal, Ligi Kuu Novemba 28, 2011
Kipigo cha 'mbwa mwizi' kilichotoka na Rooney kufunga hat-trick United ikijibu kipigo cha Manchester City cha 5-1 msimu huo. Ikiwa imeathiriwa zaidi na majeruhi na wachezaji kuwa nje wakitumikia adhabu, Arsenal ilikuwa dhoofu haswa. Hakika ilikuwa moja ya siku mbaya sana kwa Wenger kazini. "Tulivunjika nguvu kipindi cha pili, ni maumivu makubwa,"alisema kocha huyo wa Arsenal.
article-2492557-0D9C44C500000578-470_634x401_176d4.jpg
Man United 2-0 Arsenal, KOmbe la FA, Machi 12, 2011
Pamoja na Arsenal kutawala sana mchezo, mwisho wa siku walichapwa. Wauwaji siku hiyo walikwa Fabio da Silva na Rooney.
Man United 1-0 Arsenal, Ligi Kuu, Desemba 13, 2010
Bao tamu la kichwa la Ji Sung-Park lilitosha kuizamisha Arsenal mbele ya United, siku ambayo mchezaji mpya wa Gunners Marouane Chamakh alipoteza nafasi nzuri.
Man United 2-1 Arsenal, Ligi Kuu, Agosti 29, 2009
Siku hiyo Arsenal walianza vizuri, Andrey Arshavin akitangulia kuwafungia bao la kuongoza. Bao lilisawazishwa baada ya kipa Manuel Almunia kumchezea rafu Rooney kwenye eneo la hatari aliyekwen kufunga kwa penalti. Abou Diaby akajifunga mwenyewe dakika tano baadaye kuipa United bao la ushindi. Wenger akapandishwa jukwaani baada ya kutupa chupa dakika ya 95, kufuatia bao zuri la kusawazisha lililofungwa na Van Persie kukataliwa akiambiwa aliotea.
Man United 0-0 Arsenal, Ligi Kuu Mei 16, 2009
Arsenal ilikwenda Old Trafford kwa lengo la kuwabania United wasitwae taji mapema, baada ya kuwa tayari wamebeba taji la Ligi ya Mabingwa mwezi uliotangulia. Lakini pamoja na yote, United walipata ponti waliyoihitaji kubeba taji la 11 la Ligi Kuu wakiwa wamebakiza mechi moja – pia wakafikia rekodi ya Liverpool kutwaa mtajai 18 jumla ya ligi hiyo tangu inaitwa Daraja la Kwanza.
Man United 1-0 Arsenal, Ligi ya Mabingwa, Aprili 29, 2009
Arsenal walikuwa wenye bahati sana kufungwa bao moja siku ambayo United walishindwa kutumia vizuri nafasi walizotengeneza kwa matunda ya kucheza vizuri. Timu ya Ferguson ilipeleka sukrani zake kwa John O'Shea kuwasogeza jirani na fainali ya Ligi ya Mabingwa. Arsenal ilitumai kuzinduka katika mchezo wa marudiano nyumbani, lakini siku hiyo hawakufanya kosa baada ya kukifumua kikosi cha Wenger mabao 3-1 na kuifuata Barcelona katika fainali.
Man United 2-1 Arsenal, Ligi Kuu, Aprili 13, 2008
Arsenal ilipata nafasi lakini ikashindwa kuitumia kuimaliza United, baada ya Adebayor kuwafungia bao la kuongoza dakika mbili baada ya mapumziko ingawa mkono ulihusika katika bao hilo hilo. United ilisawazisha kupitia kwa Ronaldo kwa penalti baada ya William Gallas kuunawa mpira kwenye eneo la hatari, kabla ya Owen Hargreaves kuifungia United bao la ushindi kwa shuti la mpira wa adhabu umbali wa mita 25 na kuifanya ipae kileleni kwa pointi sita zaidi.
.
Man United 4-0 Arsenal, Kombe la FA, Februari 16, 2008
Ferguson aliamua kuwapumzisha Ronaldo na Ryan Giggs, lakini Rooney alitosha kuwamaliza akifunga bao la kwanza wakati Darren Fletcher alifunga mawili na Nani moja. Rooney alijitengenezea nafasi katika kikosi cha kocha wa England wakati huo Fabio Capello, huku United ikitinga Robo Fainali, ambako kwa bahati mbaya walitolewa na Portsmouth walioibuka mabingwa.
Man United 0-1 Arsenal, Ligi Kuu Septemba 17, 2006
Baada ya kucheza mechi tatu bila kushinda tangu mwanzo mwa msimu, Arsenal ilizinduka zikiwa zimebaki dakika tano mchezo kumalizia, Fabregas alipompokonya mpira Cristiano Ronaldo kabla ya kumpasia Emmanuel Adebayor ambaye alimtungua Tomasz Kuszczak. Pamoja na hayo mwisho wa msimu, United iliibeba taji kutoka kwa Chelsea huku Arsenal ikiachwa kwa ponti 21 nafasi ya nne.
Man United 2-0 Arsenal, Ligi Kuu, Aprili 9, 2006
Mabao ya Rooney na Ji-Sung Park yalitosha kuimaliza Arsenal huku United ikiweka rekodi ya kushinda mechi a tisa mfululizo katika ligi.
Man 1-0 Arsenal, Kombe la Ligi, Desemba 1, 2004
Manchester United kwa mara nyingine waliitambia Arsenal iliyokuwa imesheheni makinda waliosajiliwa na Wenger kama Robin van Persie wakati Ferguson alikuwa ana wakali kama Eric-Djemba Djemba na Kleberson. Mchezaji mwingine ambaye hakufika mbali, David Bellion, ndiye aliyefunga bao hilo pekee sekunde ya 19.
Man United 2-0 Arsenal. Ligi Kuu Oktoba 24, 2004
Van Nistelrooy alitangulia kufunga dakika ya 72 kwa penalti, na Rooney akafunga la pili dakika ya 90 kumaliza rekodi ya Arsenal kutofungwa ndania ya mechi 49.
Man United 0-0 Arsenal, Ligi Kuu Septemba 21, 2003
Mechi kali ndani ya Old Trafford. Baada ya dakika 80 mechi ilichafuka baada ya Ruud van Nistelrooy kuonyeshana ubabe na Patrick Vieira. Kisha katika dakika za lala salama Van Nistelrooy alikosa penalti baada ya Martin Keown kumchezea rafu Diego Forlan.
article-2492557-003F41F41000044C-926_634x489_1eef2.jpg
Hiloo: Martin Keown akimzomea Ruud van Nistelrooy baada ya Mholanzi huyo kukosa penalti
Chanzo:bongostaz.blogspot.com

No comments:

Post a Comment