Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, November 3, 2013

MBOWE AHANI MSIBA WA MAREHEMU ZAMBERI NGOBAI


Mhe. Freeman Mbowe akimpa pole mke wa marehemu Albertha Zamberi. Aliyevaa shati la kitenge pembeni yake ni kijana mkubwa wa marehemu Emmanuel Ngobai.
Freeman Mbowe akibadilishana mawazo na kupata maelezo kutoka kwa kijana mkubwa wa marehemu Zamberi Ngobai Mwisarya aitwaye Emmanuel Ngobai.
Leo tarehe 03/11/2013 Mhe Freeman Mbowe alifika katika Wilaya ya Bunda kuhani msiba wa Mzee Zamberi Ngobai aliyekuwa Diwani wa Kata ya Nyasura iliyoko Bunda Mjini kwa tiketi ya CHADEMA.
Diwani huyo alifariki dunia tarehe 28/10/2013 akiwa katika hospitali teule ya Bugando ambako alilazwa kwa matatizo ya ugonjwa wa Kiharusi.
Mhe Freeman Mbowe aliongozana na msafara mkubwa wakiwemo, Mhe. Lwakatare, Esta Matiko (Mb), Meshack Opulukwa (Mb), Recho Mashishanga (Mb), John Mrema na viongozi wa Mkoa na wa Kanda. Familia ya marehemu imeshukuru kwa jinsi ambavyo chama kilionesha ushirikiano mkubwa tangu ugonjwa hata mauti.

No comments:

Post a Comment